23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Museveni aipongeza CCM kwa kujenga uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Uganda

Anna Potinus

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amepongeza juhudi za Chama cha Mapinduzi CCM, katika kuleta uhusiano mzuri uliodumu kwa kipindi kirefu kati ya Tanzania na Uganda ambapo amesema changamoto waliyonayo kwa sasa maendeleo, utajiri na kazi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 13, baada ya kuwasili nchini kwa ziara binafsi ya siku moja mbapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Chato, mkoani Geita.

“Tanzania ilichangia kiasi kikubwa kuleta amani Uganda wakati Idd Amini alipohamia Kagera tulishirikiana na kumtoa ndio maana umesikia nchi hizi zina amani kwa muda mrefu kutokana na jitihada za chama cha TANU,”

“Idadi ya watu imeongezeaka ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, wakati wa uhuru Tanganyika ilikuwa na watu milioni tisa sasa ni milioni 55, Uganda walikuwa watu milioni 6 sasa wako watu milioni 44 hivyo changamoto ya leo ni maendeleo, utajiri na kazi,” amesema.

“Nikija Tanzania ni kama ninakuja kwenye hija, kisiasa hija yangu ni hapa, kama ilivyo kwa waislamu wanavyokwenda Macca kuhiji, wakatoliki wanakwenda Roma, sisi wapigania uhuru tunakuja Tanzania ndio maana nikija hapa nakuwa nimekuja kwenye hija ya kihistoria na kisiasa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles