31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili yapokea msaada wa kipimo cha macho chenye thamani ya milioni 100

TUNU NASSOR – DAR ES SALAAM

Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea kipimo cha macho (OCT) chenye thamani ya zaidi ya sh milioni 100 kutoka shule ya kufundisha kwaya ya Westminster Cathedral Choir School iliyopo London nchini Uingereza.

Akizungumza wakati wa kupokea mashine hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Laurence Museru, amesema mashine hiyo itarudisha huduma ya upimaji wa macho ambayo ilikosekana baada ya iliyokuwapo awali kuharibika.

“Tunashukuru kwa msaada huu na tunaahidi tutaituimia ipasavyo hii mashine na kuitunza ikae muda mrefu ili kuepukana na adha iliyotukumba kipindi cha nyuma”amesema profesa Museru.

Naye Daktari Bingwa wa Macho, Dk. John Kisimbi amesema mashine hiyo itapunguza usumbufu kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakienda hospitalini hapo na kukosa huduma.

“Hapo awali kulikuwa na hii mashine ila ikaharibika na kufanya kushindwa kutoa huduma hii lakini kupitia hii mashine imefanya huduma irudi tena kwani kipimo hichi kinasaidia kutambua tatizo lililopo nyuma ya jicho ambalo haliwezi kuonekana kwa macho ya madaktari” amesema Dk. Kisimbi.

Kwa upande wake Mwalimu wa shule hiyo ya kwaya ,Mathew Wright, amesema wameamua kutoa msaada huo ili kusaidia kurahisisha matibabu ya macho.

“Duniani sisi ni wamoja hivyo kupitia msaada huu utaleta ushirikiano baina ya sisi na nyinyi na ni vizuri kumuhudumia mtoto kwa kuwa ni taifa la kesho”amesema Wright.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles