24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Muhimbili yafanikiwa kutenganisha mapacha walioungana

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam  



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefanikiwa kufanya upasuaji wa kutenganisha mapacha walioungana, waliozaliwa Kisarawe mkoani Pwani, Julai 12, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 26, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Laurence  Moselu,  amesema upasuaji huo uliofanyika Septemba 23, kwa mafanikio ambapo mapacha hao wanaendelea vizuri.

“Tulifikiri kwamba upasuaji huu ungekuwa mgumu lakini tumefanikisha na tuna ‘theatre’ mbili zinazofanya upasuaji kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitatu na unafanyika kila siku na hii imepunguza msongamano wa watoto kusubiria upasuaji, wanaweza kufanya upasuaji mara 10 kwa wiki,” amesema Moselu.

Naye Daktari bingwa wa upasuaji kwa watoto Dkt. Petronila Ngiloi amesema mapacha hao walizaliwa na mama yao aitwaye Esta (22) nyumbani kwao Kisarawe, alikozalishwa na mkunga wa jadi na baada ya kugundua  watoto wameungana walipelekwa Kituo cha Afya cha Kibaha na baadaye kuhamishiwa Muhimbili wakiwa wamechoka sana.

Amesema watoto hao walipochunguzwa iligundulika wameungana sehemu kubwa ya ini na ikaonekana upasuaji huo unaweza kufanyika MNH ambapo walifanya kazi ili kuona mama huyo anapata huduma nzuri na watoto nao walitibiwa na wakawa na hali nzuri na walikuwa na uzito wa kilo  mbili kila mmoja.

“Wakati wanatenganishwa walikuwa na kilo tisa  ambapo mmoja alikuwa na kilo nne na mwingine alikuwa na kilo tano ambaye alikuwa mkubwa kuliko mwenzie na upasuaji ulifanyika kwa mafanikio na sasa hivi wanaendelea vizuri.

“Tunafanya upasuaji huu kwasababu watoto wanapoungana, tunawatenganisha ili kila mmoja awe na maisha huru lakini pia kuzuia mwingine kupata tatizo pale mmoja wao anapopata tatizo au hata kifo,” amesema Ngiloi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles