27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa siku moja aambukizwa virusi vya Corona

Beijing, China

MTOTO mchanga nchini China ameambukizwa virusi vya corona saa 30 baada ya kuzaliwa.

Kisa hicho kinaandika rekodi ya mtoto mchanga zaidi kuwahi kurekodiwa.

Mtoto huyo alizaliwa Februari 2 katika hospitali moja ya mjini Wuhan, ambako ndiko kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.

Mama wa mtoto alikutwa na virusi hivyo kabla ya kujifungua.

Haijulikani ni kwa namna gani kichanga hicho kiliambukizwa.

Shirika la habari la China, Xinhua limeripoti taarifa za maambukizi hayo juzi Jumatano.

Ilieleza kuwa mtoto huyo aliyekuwa na uzito kilogramu 3.25, alikuwa na hali nzuri na alikuwa akifanyiwa uchunguzi.

Wataalamu wa afya wanasema inawezekana ni maambukizi yaliyotokea tumboni.

”Hii inatukumbusha kuwa makini kuwa kuna uwezekano kukawa na maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.” Daktari wa hospitali ya watoto kitengo cha dawa, Zeng Lingkong aliliambia shirika la habari la Reuters.

Lakini pia inawezekana mtoto aliathirika baada ya kuzaliwa na kuwa karibu na mama yake.

”Inawezekana kuwa mtoto alipata maambukizi kwa njia za kawaida- kwa kuvuta hewa iliyotoka kwa mama alipokohoa,” daktari wa magonjwa ya maambukizi Stephen Morse ameeleza.

Watoto wachache sana wamegundulika kuwa na virusi vya corona katika mlipuko wa hivi karibuni, sawa na aina nyingine ya maradhi ya Sars na Mers.

Ripoti ya jarida la kitabibu limesema wastani wa umri wa wagonjwa ni kati ya miaka 49 na 56, kwa upande wa watoto ni mara ”chache sana”.

Vivyo hivyo, wakati wa mlipuko wa Mers mwaka 2016, Jarida la afya kuhusu maradhi ya watoto lilisema kuwa virusi vilikuwa vikiwaathiri watoto kwa nadra sana, hata hivyo sababu hazijulikani.

Mtoto wa miezi sita nchini Singapore aligundulika kuwa na virusi vya corona , halikadhalika mtoto wa miaka minane aligundulika kuwa na virusi hivyo mjini Wuhan, ambaye kwa sasa yuko Australia.

Virusi hivyo vimesambaa nje ya China tayari mataifa 27 yamethibitisha kuwa na visa 191 vya maambukizi na vifo viwili pekee nje ya China.

MAELFU WATENGWA

Wakati huo huo maelfu ya watu wameendelea kuwekwa kwenye karantini ndani ya meli mbili za abiria nchini Japan na Hong Kong, kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

Katika meli ya abiria nchini Japan, watu wengine 10 wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo na hivyo kuongeza idadi ya walioambukizwa kwenye meli hiyo kufikia 20, na kufikisha idadi jumla ya walioambukizwa nchini Japan kuwa 45.

Haya yanajiri wakati maofisa wa afya wakisema jana kuwa idadi ya vifo kutokana virusi hivyo imeongezeka kupindukia watu 500.

Takriban abiria 3,700 na wahudumu wa meli ya Diamond Princess, wamewekwa kwenye karantini Pwani ya Yokohama, kusini mwa mji wa Tokyo. Jumamosi, abiria mmoja aliyeshuka kwenye meli hiyo, alithibitishwa kuwa na virusi hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles