24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘MTOTO WA NYANI’ KUHUKUMIWA AGOSTI 21

Na WAANDISHI WETU


KESI ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka tisa inayomkabili, Baraka Joshua maarufu mtoto wa nyani inatarajiwa kutolewa hukumu Agosti 21, mwaka huu.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Catherine Kiyoja akiongozwa na Wakili wa Serikali, Florida Wenslaus baada ya kufunga ushahidi wa pande zote.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kubaka na kulawiti mtoto wa miaka tisa, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kimanga.

Joshua anadaiwa kutenda kosa hilo, Mei 17, mwaka jana katika eneo la Shule ya Msingi Tabata Kimanga, ambapo alimbaka na kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo.

Katika moja ya ushahidi uliowahi kutolewa mahakamani hapo, ulieleza kuwa , Joshua  anadaiwa kumwingilia kinyume na maumbile, mtoto huyo mara kwa mara.

Shahidi huyo, Eveline Nzagwi (42) ambaye ni Daktari Msaidizi  wa Zahanati ya Tabata Shule, alidai kuwa alibaini musuli inayokaza sehemu ya haja kubwa ya mlalamikaji ikiwa imelegea kutokana na kuingiliwa mara kwa mara.

Dk. Nzagwi ambaye ni shahidi wa tano katika kesi hiyo, alidai Mei 19, 2016  akiwa hospitali , alifika mama wa mlalamikaji akiwa na mtoto wake (mlalamikaji) akilalamika kuwa mtoto wake amebakwa.

Shahidi huyo ambaye ana uzoefu wa miaka mitano katika fani ya udaktari, alieleza kuwa baada ya kumpima  sehemu ya uke ya mtoto huyo aligundua kuwa  bikra yake ipo, lakini  uke wake ulikuwa umefunguka  kutokana na kuchezewa.

“Yule mtoto tulimpima vipimo vyote ikiwemo kipimo maalumu cha kupima sehemu za siri na kukuta hana maambukizi na hajaingiliwa ukeni.

“Lakini tulivyompima sehemu ya haja kubwa tuligundua  kuwa sehemu hiyo ina uwazi mkubwa kiasi kwamba hata ukiingiza vidole viwili vinapita bila tatizo lolote na hapo tukabaini kuwa mtoto huyo alikuwa anaingiliwa kinyume na maumbile yake kila mara” alidai shahidi huyo na kuongeza.

“Kwa hali ya kawaida sehemu ya haja kubwa huwa inakuwa na misuli iliyokaza ambayo husaidia kuzuia kinyesi kutoka, lakini endapo mtu akiwa anaingiliwa kinyume na maumbile misuli hiyo hulegea na kuwa na uwazi mkubwa kiasi kwamba hata kinyesi kinaweza kutoka bila kukizuia kutokana na uwazi uliopo” alidai Dk Nzagwi.

Inadaiwa kuwa, Joshua aliwahi kuishi na nyani baada ya kuzaliwa na kutupwa porini takribani miaka nane iliyopita katika pori lililopo mkoani Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hayo Maisha Ya Kinyani Aliyowahi Kuishi Huenda Yalimhathiri Kisaikolojia So Acha Aende Jela Akajifunze Ubinadamu. Misarable Life. Pole Kwa Mtoto

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles