Imechapishwa: Mon, May 7th, 2018

MTOTO WA MICHAEL JACKSON AMWANIKA MPENZI WAKE

CALIFORNIA, MAREKANIMTOTO wa marehemu Michael Jackson, Prince Jackson, amemwanika mpenzi wake kwa mara ya kwanza, baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa mwaka mmoja sasa.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, ameonekana mtaani akiwa na mpenzi wake, lakini hakutaka kuliweka wazi jina lake.

Kupitia ukurasa wa Instagram, aliandika: “Ninayo furaha kuweka wazi uhusiano wangu ambao kwa sasa umedumu kwa mwaka mmoja na sasa ni wakati wa kuweka wazi kila kitu.

“Tunatarajia makubwa katika uhusiano wetu kwa kipindi cha hivi karibuni na kila hatua tutahakikisha tunaiweka wazi kwa mashabiki,” aliandika Prince.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

MTOTO WA MICHAEL JACKSON AMWANIKA MPENZI WAKE