30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa miaka 15 kizimbani kwa kuchoma moto jengo la shule

AVELINE KITOMARY DAR ES SALAAM 

Wakazi wa Mbezi Jijini Dar es Salaam ,Sadiki Hassan {15} ,Hashimu Hamad {22} wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam kwa mashataka mawili ikiwemo kuchoma moto jengo la Shule.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Anifa Mwingira, Mwendesha mashtaka wa Jamuhuri Matarasa Hamisi amedai katika tarehe tofauti Aprili Mosi na Aprili 3 Mwaka huu eneo la Mbezi, Wilaya ya Ubungo washtakiwa walichoma moto mali kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili alidai katika tarehe tofauti Aprili Mosi na Aprili 3 mwaka huu eneo la Mbezi Wilaya ya Ubungo washtakiwa kwa makusudi walichoma moto jengo la shule ya sekondari Mbezi Inn kitendo ambacho ni kinyume cha sheria. 

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo,Wakili Matarasa amesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.
Hakimu Mwingira amesema dhamana iko wazi kwa kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaotoa bondi ya Sh millioni 2.

Hata hivyo washtakiwa wote walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yao itakaposomwa tena Juni 4 mwaka huu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles