31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto miaka 10 aolewa kwa Sh elfu 10 Kiteto

Na MOHAMED HAMAD-KITETO

MTOTO wa miaka kumi ambaye jina lake limehifadhiwa wa Kijiji cha Sekii Kata ya Partimbo, wilayani Kiteto mkoani Manyara, ameozwa kwa mwanaume na kuishi naye kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mtoto huyo aliozeshwa na wazazi wake,ambao ni baba na mama kwa mahari ya Shilingi elfu kumi kisha sherehe kufanyika nyumbani kwao na kwenda kuishi na bwana huyo.

Akizungumza na gazeti hili, Mratibu wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la KIWOCOA, Mwadawa Ally ambaye anaishi na mtoto huyo kwa sasa alisema mtoto huyo alitoroka kwa mume huyo aliyejulikana kwa jina la Baraka Melau  mwenye umri wa miaka 48.

“Baada ya wazazi wangu kuchukua mahari nilikwenda kwa mume, huko nilikeketwa kuchomwa sehemu za mapajani kama alama zao kwa moto, nilinyolewa upara huku nikipata mateso mbalimbali” alisema mtoto huyo

Mwadawa alisema alikabidhiwa na Ofisa wa Ustawi wa Jamii, Jacline Barongo aliyemkuta kituo cha Polisi Kiteto ili aweze kupatiwa haki zake.

Inaelezwa baada ya suala hilo kufika kituo cha polisi wazazi wake walikimbia makazi yao na hawajulikani walipo hadi sasa.

Kwa mujibu wa Ofisa  huyo wa Ustawi wa Jamii Kiteto, Jacline alisema ukatili Kiteto ni mkubwa na wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa.

Alisema wanapokamatwa watoto wao huharibu kesi kwa kutoeleza ukweli kuhofia kutengwa na familia zao.

Mtaribu wa kitengo cha kukabiliana na ukatili shirika la Kinnapa, Agnes Robert alisema kesi zilizoripotiwa za ukatili mwaka 2017-2018 ni 75, na mwaka huu wa 2020 zimefikia 146, ubakaji 17, kutelekeza familia 24, mimba kwa wanafunzi 70, shambulio la kudhuru mwili kesi 19, kutorosha wanafunzi 9, mauaji ya kichanga 1 na kulawiti 4.

Amesema ili kufanikisha mpango huo wa kuokoa watoto dhidi ya ukatili Kiteto ni kuwa na nyumba salama ambayo itatumika kuwahifadhi watakaookolewa kutoka kwa wanaume kwani baada ya hapo wazazi huwatenga kwa kutojihusisha nao baada ya sheria kuchukua mkondo wake

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa, amekiri kukithiri kwa vitendo hivyo hasa kwa jamii ya kifugaji ambao alisema imekuwa ikiozesha watoto wadogo ili waweze kupata mali.

Alitolea mfano mwaka juzi  alisema zaidi ya watoto 280 walikusanywa na Serikali na kuanzishwa masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles