31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto aliyewekewa betri kwenye moyo atamani kuwa daktari bingwa

Mtoto Happiness Josephat (5) akionekana mwenye furaha baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Muhimbili Dar es Salaam .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa taasisi hiyo, Wakili Maulid Mohamed, Mama mzazi, Elitruda Malley , Daktari bingwa wa nusu kaputi, Angela Muhozya na Daktari wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), Kulwa Richard

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MTOTO Happiness Josephati (5) aliyefanyiwa upasuaji wa kuwekewa betri maalum kwenye moyo ambayo kitaalam inaitwa ‘pacemaker’ katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  amesema anatamani aje kuwa daktari bingwa hapo baadae.

Akizungumza na MTANZANIA katika mapumziko ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Dar es Salaam jana alisema hivi sasa anaendelea vizuri huku akimshukuru Mungu, wauguzi na madaktari waliomsaidia kufika hatua aliyo nayo sasa.

“Nikiwa mkubwa nami natamani niwe daktari bingwa ili niweze kuwasaidia watu wengi dhidi ya magonjwa kama haya yanayowasumbua, “alisema Happiness.

Naye Daktari bingwa wa nusu kaputi wa JKCI, Angela Muhozya alisema kwa sasa Happiness anaendelea vizuri wakati wowote ataondolewa ICU.

“Wakati alipoletwa mapigo yake ya moyo yalikuwa 20, hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwani anapaswa kuwa na wastani wa 60 hadi 100 kwa umri wake.

Alisema Happines alizaliwa na tatizo lakini mara nyingi hali hii huwakumba watu wazima.

“Katika uumbaji wa Mungu kwenye moyo wa mwanadamu kuna kitu kama betri ambacho huzalisha umeme na kila mmoja huzaliwa nacho lakini Happiness hakuzaliwa nacho, ” alisema.

Daktari huyo alisema kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa vifaa hivyo (pacemaker)  kwa ajili ya kuwafanyia watu upasuaji na kuomba wale wenye uwezo kujitokeza ili kusaidia kukabili changamoto hiyo.

” Vifaa hivi vinauzwa ghali na vinapatikana nje ya nchi, kuna idadi kubwa ya wagonjwa ambao ni watu wazima wanasubiri  upasuaji lakini vifaa hivyo hatuna, ” alisema

Mama wa Happiness, Elitruda Malley alisema alikuwa anazimia kila mara.

” Alikuwa anachoka haraka ilibidi tumuachishe shule, nikampeleka hospitalini wakampima wakajua tatizo la moyo wakanipa rufaa ya kuja JKCI, “alisema.

Alisema hata hivyo aliambiwa gharama za matibabu yake ni Sh milioni nane ambazo hata hivyo hakuwa nazo kwa wakati huo.

” Ilibidi nirudi Arusha kwenda kutafuta fedha hizo lakini uongozi wa JKCI walisema iwapo atatokea mfadhili watanijulisha.  Ndipo wakaja hawa madaktari wa Marekani wakanisaidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles