26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MTIFUANO WA KISIASA KUHAMIA LONGIDO

*Mahakama yatengua matokeo ya ubunge

 

Na WAANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

BAADA ya Mahakama ya Rufani Tanzania kukazia hukumu ya Mahakama Kuu ya Arusha ya kumvua ubunge Onesmo ole Nangole (Chadema), sasa ni dhahiri mtifuano wa kisiasa utahamia Jimbo la Longido mkoani Arusha ambako uchaguzi mdogo utafanyika.

Mtifuano huo unatokana na siasa za kaskazini, ambazo kwa kiasi kikubwa zimetawaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hadi mahakama inafikia uamuzi wa kutengua matokeo hayo, Chadema ndiyo ilikuwa inaongoza jimbo hilo.

Ikumbukwe katika Uchaguzi Mkuu uliopita, CCM ilipoteza viti vingi vya ubunge na udiwani katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Pia eneo hilo ni ngome ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye pia aligombea urais kupitia Chadema, anayetajwa kuongeza ushawishi katika uchaguzi huo wa marudio.

Upepo wa madiwani wa Chadema kwenye kanda hiyo na maeneo mengine kujiuzulu, ni jambo jingine linalotarajiwa kukifanya chama hicho kutumia nguvu kubwa kuonyesha bado kinakubalika eneo hilo na kwamba makada hao wanaondoka tu kwa sababu zao.

 

UAMUZI WA MAHAKAMA

Akiwasilisha hoja mbele ya jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, linaloundwa na Jaji Sauda Mjasiri, Jaji Kipenka Musa na Jaji Profesa Juma Ibrahim, wakili Method Kimomogolo alidai Jaji wa Mahakama Kuu, Sivangilwa Mwangesi hakuainisha kilichotokea katika chumba cha majumuisho kama kilikuwa ni vurugu au mzozo wa maneno.

Wakili Kimomogolo alidai kwamba katika hukumu yake, Jaji Mwangesi pia aliongeza neno ambalo halikuwa katika kuelezea kilichotokea ndani, lakini pia alijielekeza katika ushahidi wa shahidi wa tano ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Longido.

“Katika ushahidi wao, hapakuwa na ushahidi wa kufanyika vurugu, kinachoitwa vurugu bado kisingeweza kusababisha matokeo kushindwa kutangazwa,” alidai Wakili Kimomogolo.

Hoja nyingine, ilidaiwa Jaji Mwangesi katika uamuzi wake hakufafanua ni kwa vipi mazingira ya chumba cha majumuisho yaliathiri ujumuishaji wa matokeo.

Kutokana na hoja zilizowasilishwa mbele ya jopo hilo, Wakili Kimomogolo alidai kuwa ni maoni yake Jaji Mwangesi hakujielekeza vyema na ipasavyo kwenye misingi ya kisheria.

Kutokana na sababu hizo, aliliomba jopo hilo la majaji watengue uamuzi wa Jaji Mwangesi na watamke mwomba rufaa ambaye ni Nangole, alichaguliwa kihalali na arejeshewe ubunge wake.

 

CCM YAPONGEZA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole,  aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam  jana kuwa chama chao kimefarijika  kutokana na uamuzi huo.

“Tumepokea kwa faraja kubwa, kumekuwa na maneno kutoka kwa wawakilishi wa vyama vya siasa, si vyote, wenyewe huwa wanaamini mahakama ikitoa haki kwao inatenda haki, ikitoa kwa wengine haitoi.

“Tunaheshimu uamuzi wa mahakama, tunatoa rai iendelee kufanya kazi yake vizuri kwa uhuru na haki na wala isisikilize wengine.

“Tunatoa pongezi kwa wananchi wa Longindo na wanachama wa CCM, kwamba madai yao mahakama imeyathibisha,” alisema Polepole.

Kuhusu hatua inayofuata, Polepole alisema hivi sasa wanasubiri barua kutoka kwa mahakama kuhusu rufaa hiyo na baadaye vikao vya chama vitakaa.

“Baada ya vikao vya chama kukaa, tutapeleka barua Tume ya Uchaguzi, tuna imani mamlaka husika itachukua hatua haraka ili wananchi wa Longido wapate mwakilishi wao,” alisema.

 

  1. KURUSWA

Aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM ambaye alishinda rufaa hiyo, Dk. Steven Kuruswa, alisema mahakama imejidhihirisha kwa mujibu wa sheria kuwa inatenda haki.

“Ninaishukuru mahakama, haki ya mwenye haki huwa haipotei, nina imani vyombo husika vitafanya haraka ili wananchi wapate mwakilishi wao,” alisema Dk. Kuruswa.

 

CHADEMA

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, alisema kama mahakama imetoa uamuzi hawana namna zaidi ya kujipanga kwa uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles