31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtibwa yajipanga kucheza na Yanga

MTIBWA SUGARNa THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KATIKA kuhakikisha inazidi kujiweka imara, timu ya Mtibwa Sugar ina mpango wa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga, kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo wa kirafiki uliopita Mtibwa walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro wikiendi iliyopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana Ofisa Habari wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, alisema wanataka kukiimarisha kikosi chao vizuri  kupitia mechi hizo ambapo kwa sasa wapo katika maandalizi ya kukutana na timu hiyo.

“Mchezo uliopita tulifanikiwa kupata ushindi hivyo tutaendelea kujipima zaidi kwa mechi nyingine ambazo zitamsaidia kocha kufahamu mapungufu yaliyopo katika kikosi na kuyafanyia kazi, tunajipanga wiki hii mwishoni kucheza na Yanga japo hatujajua siku,” alisema.

Alisema bado wanaendelea na usajili kwa wachezaji wengine ambao wataona watailetea timu hiyo matokeo mazuri na kuzidisha ushindani katika msimu ujao wa Ligi Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles