27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mteule wa Trump azidi kuandamwa kashfa unyanyasaji kijinsia

NEW YORK, Marekani

UTAWALA wa Rais Donald Trump, umezidi kuandamwa na malalamiko kuhusu vitendo vya unyanyasaji kijinsia, baada ya mwanamke wa pili  kujitokeza akidai kufanyiwa kitendo hicho na  mteule wa kiongozi huyo katika Mahakama Kuu ya nchi hii,  Brett Kavanaugh.

Taarifa zilizopatikana mjini hapa jana zilieleza kwamba, mwanamke huyo, Deborah Ramirez, ambaye alisoma na jaji huyo katika Chuo Kikuu cha Yale aliiambia mahakama hiyo kwamba, Kavanaugh alimwonesha sehemu zake za siri wakati wakiwa bwenini madai ambayo yanakanushwa na jaji huyo.

Katika malalamiko hayo, Ramirez, anadai kwamba tukio hilo lilitokea wakati akiwa binti na wakati huo wakisoma pamoja na jaji huyo katika Chuo hicho kikuu mwaka 1983-4.

Alisema wakati anafanyiwa kitendo hicho walikuwa wakishiriki katika  mchezo wa kunywa ambapo watu wengine walikuwa wamekaa kwenye mduara wakiwaangalia.

“Nakumbuka nilielekezewa uume mbele yangu,” alisema mwanamke huyo. “Nilikuwa nafahamu si kitu ambacho nilikipenda na kiliniumiza sana akili,” aliongeza.

Ramirez alisema mbali na kuoneshwa sehemu hiyo ya siri, alidhihakiwa na kutukanwa wakati aliposema kuwa hakutaka kufanyiwa hivyo na baadaye  akaishia kugusa sehemu za siri za kiume wakati akijaribu kumsukuma mwanamume huyo.

Tuhuma dhidi ya jaji huyo zimekuja zikiwa ni hatua za mwisho kwa kigogo huyo kukabidhiwa madaraka rasmi ambapo anatakiwa kupitishwa na maseneta wa Kamati ya Wanasheria kabla ya jina lake kukabidhiwa mikononi mwa baraza zima la maseneta.

Kwa upande wake mlalamikaji wa kwanza, Profesa Christine Blasey Ford, ambaye wiki iliyopita ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Kavanaugh kuhusu kufanyiwa ukatili huo kijinsia miaka ya 1980, ameshakubali kuwasilisha ushahidi wake katika baraza hilo la maseneta Alhamisi wiki hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles