30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtatiro atakiwa kuacha malumbano

Julius Mtatiro
Julius Mtatiro

NA ESTHER MNYIKA,DAR ES SALAAM

MJUMBE wa Baraza Kuu Jumuiya ya Vijana la Chama cha Wananchi (JUVICUF), Khomein Rwihula  amemtaka  aliyekuwa Kiongozi Mwandamizi wa chama hicho Tanzania Bara, Julius Mtatiro kuacha malumbano katika mitandao ya  jamii.

Akizungumza jana na MTANZANIA,  Mjumbe wa JUVICUF, Rwihula alisema  umekuwapo mvutano unaoendelea katika mitandao ya  jamii kwa viongozi tofauti tangu Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kugombea nafasi ya uenyekiti na kurudi kuwa mwanachama.

Alisema Profesa Lipumba alijiuzulu na baada ya muda aliandika barua ya kurudi   CUF kwa mujibu wa  kifungu cha 117 katiba ya chama.

“Mtatiro amekuwa tofauti kurejea kwa Profesa Lipumba  katika chama… ndiyo huo mvutano unaendelea katika mitandao ya  jamii huku wengine wakimtaka arudi katika chama na aendelee na uongozi na wengine wapo kati,”alisema Rwihula.

Alisema hali hiyo imesababisha kuwagawanya wanachama wa CUF, viongozi na mashabiki wa chama hicho.

Aliwaomba viongozi hao kuacha mivutano hiyo  na badala yake  kujenga mikakati ya kujenga chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles