31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mtanzania Rebeca Gyumi ashinda tuzo UN

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWANAHAKATI wa haki za wanawake na wasichana Tanzania,  Rebeca Gyumi na watu wengine wawili na shirika moja la raia, wameshinda tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu

Washindi hao wametangazwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Maria Fernanda Espinosa ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza kwa mchango wao wa kusogeza mbele haki za binadamu.

Hiyo ni tuzo ya 10 ambayo mwaka huu inaendana na miaka 70 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambako washindi hao watapokea tuzo hizo tarehe      Desemba 10 mwaka huu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

Taarifa ya ofisi ya  Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa imefafanua kazi za washindi hao akitoa mfano Rebeca Gyumi.

Gyumi muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Msichana Initiative ambaye kwa miaka minane amekuwa akihoji uhalali wa Ibara ya 13 na 17 ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 na 15 kwa ridhaa ya wazazi au mahakama.

Taarifa hiyo inasema, “ Gyumi alishinda kesi hiyo mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzaina mwaka 2016.”

Mshindi mwingine ni Asma Jahangir mwanaharakati mwanasheria wa Pakistani ambaye amefariki dunia mwaka  huu.

Jahangir kwa miongo mitatu amekuwa akitetea haki za wanawake, wasichana, watoto na makundi madogo ya dini na maskini nchini mwake na alifungua kituo cha msaada wa sheria.

Hatya hivyo alikuwa akikumbwa na misukosuko lakini alikuwa na uwezo wa kushinda kesi zilizokuwa na utata.

Mshindi  mwingine,  Joênia Wapichana au Joênia Batista de Carvalho, mwanaharakati wa haki za watu wa jamii ya asili, Brazil, ni mwanamke wa kwanza wa jamii hiyo kuwa mwanasheria.

Nalo shirika la Front Line Defenders Ireland ambalo linachechemua na kulinda haki za binadamu nchini Ireland linahusika na kulinda mahitaji ya watetezi  waweze kuendelea na kazi zao bila hatari, vitisho wala kukamatwa.

Tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa hutolewa kwa watu binafsi na mashirika kwa kutambua mchango wao wa pekee katika kuendeleza na kulinda  haki za binadamu na uhuru wa msingi wa binadamu kwa mujibu wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha tuzo hiyo kwa azimio la Desemba 10,  1968 wakati tamko la haki za binadamu lilipotimiza miaka 20 tangu kupitishwa.

Tuzo imetolewa mwaka 1973, 1978, 1988, 1993, 1998, 2003, 2008 na 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles