23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtangazaji anayeshitakiwa kwa mauaji  asimulia kilichojiri

NAIROBI, KENYA

MTANGAZAJI maarufu wa televisheni nchini hapa, Jacque Maribe, ameeleza kilichojiri baina yake na rafiki yake wa kiume, Joseph Kuria Irungu usiku wa mauaji ya mfanyabiashara, Monica Kimani.

Katika kesi inayowakabili wawili hao, waendesha mashitaka walijumuisha taarifa iliyotolewa na Maribe, akieleza kilichojiri usiku wa mauaji.

Alisema Irungu maarufu kama Jowie alikuwa akiomba radhi kwa kitu, ambacho hakukielewa.

Anajieleza: nina umri wa zaidi ya miaka 18 naweza kusoma na kuandika. Taarifa hii iko kwa Kiingereza. Naitoa kwa kadiri ya nijuavyo na nimaamini iwapo itawasilishwa mahakamani kama ushahidi naweza kushitakiwa ikibainika nimesema uongo au kitu kisicho na ukweli.”

Hivyo, mimi mtajwa hapo juu, Mkenya mwenye umri wa miaka 30. Nafanyakazi katika Kituo cha Habari cha Royal Media Services kama mwandishi mwandamizi na mtangazaji wa habari nathibitisha maelezo haya ni ya kweli.

Maribe anaendelea kueleza hasa namna alivyokutana na Joseph Kuria Irungu maarufu kama Jowie akikiri kuwa yu mchumba wake na uhusiano wao ulianza Juni 2018.

“Mara ya kwanza niliyokutana na Jowie ilikuwa mwaka 2017 katika hafla ya Chama cha Jubilee kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya, na baadaye Kasarani, pia kwa shughuli za Jubilee.

Anaeleza kuwa wakati huo, Irungu alikuwa mlinzi wa Joyce Lay, Mbunge wa zamani wa Taita Taveta (Wanawake).

Anaeleza kuwa Jowie alikuwa akiishi Buru Buru Phase III na marafiki wake wawili.

Mbali ya kuwa mlinzi kwa viongozi wa juu, pia alifanya kazi katika kampuni binafsi ya ulinzi Dubai.

Akieleza kilichojiru usiku wa Septemba 19, Maribe anasema, alikuja akilia: alianza kuondoa nguo zake. Wakati huo, nilikuwa nimepanda kitandani. Wakati aliporudi chumbani alikuwa akilia, akiniambia kuwa anasikitika na ananipenda sana.

Nilishangaa kwa sababu hatukugombana, nilimwambia mwanangu amelala na hivyo aache makelele asije mwamsha mtoto, lakini aliendelea kulia, akisema “Jacque ninasikitika”, lakini nilimpuuza.

Kisha akatembea kuelekea chumba cha kuhifadhia vitu. Nilisikia sauti ya mlio wa risasi na niliruka kutoka kitandani na kwenda katika katika chumba hicho na kumkuta amelala sakafuni. Alikuwa na damu sehemu ya juu ya kifua kushoto.

Alikuwa akirudia kusema: “Nakupenda. ninasikitika.” Nilishtushwa na hali hiyo nikakimbilia chumbani kufuata simu yangu.

“Wakati niliporudi katika chumba hicho hakuwepo. Nilimuona kupitia dirisha kuwa alienda kwa jirani yetu, Bryan Kassaine.

Nilikimbilia nje na kumkuta Joseph Kuria Irungu amelala chini. Bryan Kassaine alikuwa ametoka nje.

Mke wa Bryan, Cate pia alikimbilia nje ambako Joseph alikuwa amelala akiwa bado anavuja damu kutokea kifuani.

Maribe anaeleza kuwa taarifa nyingine aliyoitoa kwa polisi kwenye Makao makuu ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai Septemb 28, 2018, ikitaja wapi alipokuwa na shughuli alizofanya Septemba 19, 2018, siku ambayo Kimani aliuawa zinabakia kama zilivyo.

Maribe anashitakiwa kwa mauaji hayo kwa kile kinachodaiwa alifahamu na kujaribu kuficha uhusika wa mchumba wake huyo katika mauaji hayo.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo baada ya kuahurisha juzi, ambapo washitakiwa hao ambapo walikana mashitaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles