23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mtandao hatari wa majambazi wanaswa

DSC_4756NA HERIETH FAUSTINE, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limebaini na kuwakamata majambazi watatu wakiwa na silaha 28 risasi 835 pamoja na vifaa mbalimbali vya jeshi hilo,  ambavyo walikuwa wakitumia kufanyia  uporaji katika maeneo mbalimbali jijini hapa.

Vifaa vingine ni pamoja na makoti matatu ya kuzuia risasi (bulletproof) , sare za polisi, pingu 12 pamoja na radio 12 za upepo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simoni Sirro, alisema jana kuwa uchunguzi huo ulifanyika kupitia kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha kwa zaidi ya wiki tatu na kubaini kuwa majambazi hao ndio waliokuwa wakifanya  matukio ya uhalifu katika mabenki mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Alisema tukio la Agosti 28 mwaka huu katika Jengo la Sophia House, majambazi 10 walivamia Ofisi za Matrix International Company wakiwa wamevalia sare za jesi hilo na kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia gari ya Noah yenye iliyokuwa na namba za bandia.

“Mnamo Agosti 29 mwaka huu majambazi wapatao 10 waliingia katika jengo la Sophia House maeneo ya Veta  Chang’ombe na kuvamia Ofisi za Matrix Intenational Company wakiwa wamevalia  sare za polisi na kuwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kupiga risasi moja na kumuamuru Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jerry Oge ambaye ni Mchina aonyeshe fedha za mauzo na ndipo walipora  milioni 35 na baadaye kutoweka kwa kutumia gari ya Noah yenye namba T549 BPK ambazo ni bandia,”alisema Kamishna Sirro.

Alisema baada ya tukio hilo pamoja  na lile lililotokea katika Benki ya CRDB tawi la Mbande na kusababisha polisi wanne kuuawa. “Timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu iliweka mtego ambapo iliweza kuwakamata majambazi watatu katika maeneo ya Mbagala, Keko pamoja na Kawe,” alisema.

Alisema majambazi hao walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kutaja silaha walizonazo pamoja na kuwapeleka askari eneo la Mbezi Chini kwenye nyumba waliyoikodi.

“Baada ya kufanya upekuzi katika nyumba hiyo tulikuta silaha za kijeshi aina ya SMG 3, magazine tupu nane na risasi 120, shot gun pump action tatu zikiwa na risasi 130, bastola 16, magazine tupu moja, risasi 548, radio Call 12, chaja za radio call 3, darubini tatu.

“Vitu vingine ni pingu za plastik 45, makoti ya kujikinga na risasi matatu, mkasi mmoja wa kukatia  vyuma vigumu, mtalimbo mmoja wa kuvunjia milango, risasi baridi za kutishia 37,Tool Box moja ya kusafishia silaha.

“Vingine ni nyundo kubwa moja, pingu za  chuma tatu, mashine ya kuhifadhia kumbukumbu (CCTV) server), panga moja,gari no. T.950DGC Toyota Noah rangi ya Silver pamoja na Toyota ALPHAD T.987 CLH,”alisema Kamishna Sirro.

Aidha katika mkutano huo, Kamishna Sirro alisema baada ya mahojiano na watuhumiwa hao wa ujambazi waliksema silaha hizo wamekuwa wakiziagiza kutoka nchi ya Burundi pamoja na Afrika Kusini  huku silaha zingine wakiwa wamezificha katika Msitu wa Vikindu uliopo Mkuranga mkoani Pwani ambapo polisi waliingia katika pori hilo huku wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa hao.

“Tulifanya upelelezi na kugundua walifanya mtego, nasi tuliamua kuwatanguliza wao, wakiwa ndani ya msitu ghafla walisikia milio ya risasi ikitokea mbele ambapo askari walilala chini na kusikika sauti zikisema ‘mmetua sisi’.

Baada ya mfululizo wa risasi askari walishuhudia majambazi hao ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zikipigwa wakiwa wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi,”alisema.

Alisema askari waliwabeba majambazi hao kwenye gari kuelekea hospitali, lakini wote walifariki dunia wakiwa njiani kutokana na kutokwa na damu nyingi.

Katika tukio jingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni liliwakamata watuhumiwa wanaovunja nyumba usiku na kupora mali mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles