24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

MTANDA AWATAKA WAKULIMA WABADILIKE

Na IBRAHIM YASSIN-NKASI


WAKULIMA wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wameshauriwa kubadilika na kuacha kulima maeneo makubwa bila kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo. 


Ushauri huo umetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda,  alipokuwa akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Ntatumbila wakati wa madhimisho ya siku ya wakulima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Ruvuma Commercialization Diverstation (Rucodia) yakiwa na lengo la kujenga mtandao wa wakulima wilayani humo.

Alisema wengi wao bado wanalima kizamani bila kufuata kanuni bora za kilimo, huku wakiamini kulima maeneo makubwa ndiyo kupata mazao mengi.


Alisema wakulima wilayani humo wamekuwa wakilima mashamba makubwa bila kuwa na uwezo wa kununua pembejeo za kilimo na kuyahudumia kwa palizi na viuatilifu.


Akitoa taarifa ya mradi wa kutengeneza mtandao wa kuwajengea uwezo wauza pembejeo za kilimo na mifugo, Filbeth Misigalo, alisema mradi huo umeanzishwa katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera na kufadhiliwa na Shirika la Alliance for Green Africa (AGRA).


Alisema mradi huo unatekelezwa katika wilaya za Nkasi, Mpanda, Mlele, Kigoma Vijijini, Kigoma Mjini, Ngala na Biharamulo.
Alisema lengo ni kupata mawakala 50 kwa kila wilaya ambao watakuwa wakiuza pembejeo hizo ili kukabiliana na wimbi la pembejeo bandia.


Alisema walishirikiana na makampuni ya mbegu ya Meru, Ifad Seed pamoja na Agri seed waliotoa mbegu za mahindi aina tofauti zilizotumika katika mashamba darasa hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles