27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MTAHINIWA FEKI JELA MIAKA MITATU

Na FARAJA MASINDE  -DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, Miraji Saidi, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya udangantifu kwenye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.

Hukumu hiyo ilitolewa jana   na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan baada ya kujiridhisha na hoja za   mashahidi   watano wa upande wa mashtaka, bila kuacha shaka yoyote.

Hakimu Hassan alisema  vitendo hivyo vya kufanyia watu mitihani ndivyo vinavyosababisha uzembe na hasara kubwa kwa taifa.

Hivyo alitoa adhabu hiyo   ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

“Mahakama imekutia hatiani mshtakiwa, hivyo kwa kosa la kwanza ninakuhukumu kwenda jela miaka mitatu, kosa la pili jela miaka miwiwli na kosa la tatu utatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

“Hivyo jumla utatumikia kifungo cha mikaa mitatu ili iwe onyo na funzisho kwa wote wenye tabia kama hiyo,” alisema Hakimu Hassan.

Awali,   Wakili wa Serikali, Grace Mwanga, alidai   kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshatakiwa na hivyo kuiomba mahakama   kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

Katika utetezi wake, Miraji aliomba apunguziwe adhabu.

Miraji ambaye ni mkazi wa Ubungo, alikabiliwa na mashtaka matatu na katika shtaka la kwanza inadaiwa kuwa katika tarehe isiyofahamika, 2016 akiwa Ukonga alikula njama na kudanganya picha ya utambulisho (pasipoti) ya kuhitimu mtihani wa elimu ya sekondari mwaka 2016.

Katika shtaka hilo, Miraji anadaiwa kubadilisha picha halisi ya Emmanuel Hungo, iliyokuwa imesajiliwa kwa namba P. 3890-0039 na Necta ambako alii-‘scan’ picha yake na kisha kuiziba picha halisi kuonyesha kwamba fomu hiyo ilikuwa imekosewa jambo ambalo si kweli.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa Novemba 11, 2016 Shule ya Sekondari Lilisia iliyoko ndani ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, alifanya udanganyifu wa  picha hiyo kwa kuonyesha kwamba alikuwa ni miongoni mwa watahiniwa waliopitishwa na Necta kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kuanzia Novemba 1, 2016 akiwa na namba P. 3890-0039, jambo ambalo si kweli.

Na katika shtaka la tatu, Novemba mosi, 2016 katika Shule ya Sekondari Lilisia ndani ya Manispaa ya Ilala, alidanganya kwa kujitambulisha kwa msimamizi wa mitihani,   Jackline Michael, kuwa yeye ndiye Emmanuel Huago, aliyesajiliwa na Necta kwa namba P 3890-0039,  jambo ambalo si kweli

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles