27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtafiti abuni kitasa kinachofunguliwa na simu

CHRISTINA GAULUHANGA – DA ES SALAAM

Mtafiti kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Filbert James, amebuni kitasa cha mlango wa nyumba kinachofunguliwa kwa simu ya mkononi ili kukomesha utumiaji funguo bandia.

Akizungumza na MTANZANIA katika Maonyesho ya Sabasaba leo Jumamosi Julain 6, Filbert amesema kukamilika kwa mfumo huo kutasaidia pia kuepukana na suala la uvunjaji kufuli.

Amesema mfumo huo unasaidia kufungua geti la mlango unaotembea ambapo mtumiaji akishaingia geti hujifunga lenyewe.

“Ili kupata mfumo huu ni la lazima uwe na mlango wa kutembea na mota halafu unaingiza simu kadi ambayo ndio itakuwa inakuruhusu kama unafahamu namba yake ya simu na ukichukua namba nyingine kiholela inagoma hadi ile uliyoitambulisha kwenye mfumo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles