29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mstaafu Tanga aisababishia serikali hasara ya Sh milioni 30

Oscar Assenga, Tanga

Taasis ya kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani wa Tanga imemtaka aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Idara ya Elimu, Aneth Makame kurejesha kiasi cha Sh milioni 30 alizochukua wakati akijua tayari amekwisha kustaafu na kuisababishia serikali hasara.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Takukuru Mkoa, Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya utendaji wao ambapo katika kipindi hicho walifungua shauri moja ambalo lilifikia mwisho na
kutolewa maamuzi.

Amesema mtumishi huyo aliomba kustaafu kwa hiari akiwa na miaka 55 lakini akaendelea kuchukua mshahara kwa miaka mitano iliyofuatia na hivyo kuisababishia serikali ya kiasi hicho kwa serikali huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Mariba amesema bado mtumishi huyo hajaanza kurejesha fedha hizo huku taasisi hiyo ikimtaka kufika ofisini kwao yeye na familia yake ili waweze kuweka utaratibu wa kuzirejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo.

“Endapo atashindwa kufanya hivyo basi itabidi tutafute utaratibu mwengine kupata fedha hiyo na hii itakuwa ni pamoja na kuuza nyumba au mali yoyote anayomiliki, kabla ya maamuzi hayo mshtakiwa alikuwa
amekwisha kukaa mahabusu takribani mwaka mmoja na nusu bila dhamana”amesema Mariba.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo amesema katika kipindi hicho mkoa huu umeokoa kiasi cha sh.milioni 2,190,500 kilicho kuwa kimechukuliwa kinyume cha sheria na taratibu za fedha .

“Pamoja na kiasi hicho kurejeshwa tumewaandikia barua waajiri wa wahusika kwa lengo la kuweza kuchukua hatua za kinidhamu na kiutawala
dhidi ya watumishi waliohusika na matendo hayo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles