24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MSONGO WA MAWAZO MAENEO MENGINE YA MAISHA

  1. Umasikini na kiwango kidogo cha elimu

Umasikini na kiwango kidogo cha elimu mara nyingi vina uhusiano na vinaweza kuwa chanzo cha msongo wa mawazo.

Umasikini na kiwango kidogo cha elimu au pasipo na elimu kabisa vina uhusiano wa karibu sana na hali mbaya ya afya. Mara nyingi katika maeneo mengi, watu wenye elimu kubwa wamekuwa na afya bora pia.

Umasikini husababishwa na mambo mengi ikiwemo uzee, kutosoma, kutengwa, kubaguliwa, kipato kidogo, mtazamo wa jamii juu ya jinsia fulani, mfano; katika jamii nyingi mwanamke hunufaika kidogo na hategemewi kumiliki mali. Hii inawafanya wanawake wazee ambao ni masikini kuwa wengi katika jamii nyingi kuliko wanaume wazee masikini.

Mbali na kiwango cha elimu, yako maeneo mengine yanayoweza kuchangia katika umasikini na kuleta sana msongo wa mawazo kama vile;

  • Mtu mlemavu ambaye anakataliwa kote anakoomba kazi kwakuwa tu inaaminika hataweza kufanya kazi kutokana na ulemavu wake, lakini ikumbukwe kuwa wapo walemavu wafanyao kazi kwa bidii na kwa ufanisi sana mara nyingine hata kuliko wale walio wazima.
  • Mtu mwenye umri wa miaka 45 na kuendelea anayekataliwa kazini kwa sababu tu waajiri wanaogopa kuajiri mtu atakayestaafu karibuni.
  • iii)   Msichana wa umri wa kati anapokataliwa na waajiri, wakiogopa  kumwajiri kwa maana ataweza kupata ujauzito wakati wowote.

Hali hizi zote huleta msongo wa mawazo na maumivu makali moyoni, hali ambayo huweza kuathiri afya na hali nzima ya maisha ya mwathirika.

  1. Hali ya kukosa makazi maalumu

Hii inajumuisha watu wasio na uhakika wa mahali pa kulala na hata mahali pa kupumzika wakati wa mchana. Watu wasio na makazi maalumu wako wa rika tofauti kuanzia watoto wa umri wa miaka 18 na kuendelea. Asilimia 45 ya watu hawa wasio na makazi maalumu inachangiwa na wanaume wasio na ndoa. Familia zisizo na makazi maalumu zimeongezeka kwa kasi kutoka miaka ya 1990.

Kukosa makazi au mahali pa kulala na kuzurura mitaani kunasababishwa na sababu nyingi zikiwemo ugomvi na kutoelewana katika familia, kukosa kazi, kukosa kipato, kutengwa kwa sababu ya tabia mbovu n.k. Asilimia 22 ya wazazi wasio na makazi ni kwa sababu ya ugomvi wa nyumbani.

  1. Familia

Familia zenye nafuu kiuchumi huweza kujihudumia mahitaji ya siku, wazazi huyamudu majukumu yao kama wazazi, hawana sana matatizo ya kifedha, mavazi wala malazi, matatizo ya kiafya na ya talaka pia ni machache kwao. Tofauti na sababu hizi, familia zenye kipato cha chini huishi kinyume na hali zilizoelezwa hapo juu.

Familia zilizo bora huwawezesha watoto kuishi na baba na mama zao wa damu kwa muda mrefu na hii huwajengea watoto uwezo mkubwa wa kukabiliana na mikikimikiki ya maisha na ufanisi shuleni.

 

  1. Umri na ulemavu wa akili

Watu wenye umri mkubwa (wazee) au wenye ulemavu, hukutana na vipindi vya msongo wa mawazo vya mara kwa mara katika maisha yao ya kila siku, hasa kwa sababu ya mtazamo fulani jamii iliyonayo kuhusu wao.

Katika jamii nyingi, watu wanapokuwa na umri mkubwa hulazimika kuwapisha wenye umri mdogo waendelee na kazi na wao hutengwa, wengine huwekwa katika nyumba maalumu za watu wazee, wengine hurudishwa vijijini ili wasiwazuie wengine kiutendaji. Tofauti na nchi nyingi, Japan hutumia wazee kama chemichemi ya uzoefu na ujuzi.

Katika hali kama zilizotajwa hapo juu, mtu aliyezeeka hujiona hafai na ni mzigo katika jamii na kwa waliomzunguka, hii huleta msongo wa mawazo sana kwao. Tatizo hili ni kubwa sana katika nchi za kwetu ambako umri wa kustaafu ni mdogo (kati ya miaka 60-70).

Tukiwaangalia watu wenye ulemavu, wao huwa katika wakati mgumu zaidi, kwa sababu hudharauliwa na kutengwa na hata kutungiwa majina ya kuwadhihaki. Maumivu huwa makali zaidi pale wanapokumbuka kuwa ulemavu wao si wa leo na kesho tu, bali ni wa maisha yao yote.

Watu wengi hasa katika familia wamekuwa wakiona walemavu kama mizigo, wasio na faida na ambao huwapotezea muda wao wa kufanya mambo mengine ya maana zaidi. Ni lazima jamii ibadilike kimtazamo, iwajali, kuwapenda na kuwaheshimu walemavu, wote tukijua ya kuwa hata kama watu hawa hawana baadhi ya viungo vinavyofanya kazi au kutumika, viko vingine vinavyoweza kutumika kwa ufanisi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles