23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MSONDO NGOMA WAMEENDELEA KUONYESHA UMUHIMU WA HAKIMILIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MATUKIO yanayoonyesha umuhimu wa hakimiliki yameendelea kutokea kwenye tasnia ya burudani nchini, ambapo wiki hii tukio lingine linaloihusisha bendi  kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma na lebo ya Diamond Platnumz (WCB) limegonga vichwa vya habari.

Bendi hiyo kongwe kupitia mawakili wao, (Maxim Advocates), waliiandikia barua lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) wakiitaka ilipwe fidia ya Sh milioni 300, huku ikionyesha dhamira ya kuishtaki isipofanya hivyo ndani ya siku saba kwa kunakili kionjo cha ala ya upepo (Saxophone) kilichowahi kutengenezwa na kutumiwa na bendi hiyo katika wimbo wao wa Ajari.

Itakumbukwa Agosti 25, mwaka huu, Diamond Platnumz akishirikiana na wasanii wake wa WCB, ambao ni Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Maromboso na Lavalava, walitoa wimbo unaoitwa Zilipendwa, ambao ndani yake katika dakika 4 sekunde ya 55 hadi dakika 5 sekunde ya 10  kilichezwa kionjo cha saxophone ambacho kinafanana vile vile na kionjo kilichotengenezwa na kuchezwa na Msondo Ngoma katika dakika ya 6:38 mpaka dakika ya 6:52 ndani ya wimbo wao maarufu wa Ajari.

Wakili Mwesigwa Muhingo kupitia barua hiyo, ambayo nakala yake imepelekwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Chama cha Hakimiliki (COSOTA), aliitaka lebo ya WCB kuilipa bendi ya Msondo Ngoma kiasi hicho cha fedha haraka iwezekanavyo kwa kosa la kunakili kinyemela kionjo hicho cha kuvutia, huku wakijua ni kinyume cha sheria za hakimiliki.

Japokuwa mpaka sasa upande wa WCB hawajasema chochote, lakini suala hilo limekaa vibaya upande wao, kutokana na ukweli kuwa, lebo hiyo imenakili kionjo cha Msondo Ngoma bila ruhusa ya wenyewe.

Tukio hilo limekuwa kama mwendelezo wa matukio yanayoonyesha umuhimu wa hakimiliki kwa wasanii. Ni siku chache zimepita toka msanii Snura kuweka dhamira ya kuishtaki kampuni moja inayozalisha unga kwa kutumia wimbo wake wa Majanga katika tangazo la bidhaa yao bila ruhusa yake.

Lakini si hivyo tu, tuliona mwezi uliopita Mwana Fa na AY wakiishinda kampuni moja ya mawasiliano na kutakiwa kulipwa Sh bilioni 2.1 kwa kosa linalofanana na hilo hilo la hakimiliki, baada ya kampuni hiyo kutumia nyimbo zao mbili (Usije Mjini, Dakika Moja) bila ruhusa ya wasanii hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles