25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MSHTAKIWA MWENZA NA WAKILI MWALE AHUKUMIWA

Na JANETH MUSHI-ARUSHA


MSHITAKIWA wa pili katika kesi inayomkabili Wakili Maarufu jijini Arusha, Median Mwale (Don Bosco Gichana, raia wa Kenya), amehukumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kulipa faini ya Sh milioni 300 na kifungo cha miaka mitano jela.

Mbele ya Jaji Isa Maige, mshitakiwa huyo kati ya watuhumiwa wanne wanaokabiliwa na mashitaka hayo, Septemba 13 mwaka huu. alikiri makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili ikiwamo utakatishaji fedha haramu zaidi ya dola za Marekani milioni 5.2.

Pamoja na Wakili Mwale na Gichana, washitakiwa wengine katika shauri hilo namba 77 la mwaka jana ni Boniface Mwimbwa na Elias Ndejembi, ambao walikuwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Meru mkoani Arusha.

Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji Maige alisema baada ya kuzingatia maombi ya mawakili wa utetezi walioomba mteja wao kupunguziwa adhabu, kwa kosa la kwanza ambalo ni kula njama ya kutenda kosa, anamhukumu kifungo cha miaka mitano, ambayo inahesabiwa kuanzia siku aliyokamatwa na kuwekwa ndani   Aprili 10 mwaka 2013.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles