27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MSHAHARA WA TEVEZ KUTIKISA DUNIA

BUENOS AIRES, ARGENTINA


carlos-tevez

NYOTA wa klabu ya Boca Juniors, Carlos Tevez, anatarajia kutikisa dunia kwa kuwa mchezaji ambaye anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa katika soka duniani.

Matajiri wa nchini China ambao wanamiliki klabu ya Shanghai Shenhua, inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, wanatarajia kuonesha jeuri ya fedha kwa kutaka kumfanya mchezaji huyo awe anaongoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani.

Klabu hiyo imedai kuwa ipo tayari kumsajili mchezaji huyo kutoka Boca Juniors na kumlipa kitita cha pauni 615,000 kwa wiki na kuvunja rekodi za mishahara kwa wachezaji.

Kwa sasa wachezaji ambao wanaongoza kwa kulipwa fedha nyingi kwa wiki ni Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ambao wote wanachukua kitita sawa cha pauni 365,000 kwa wiki, huku wakichukua kitita cha pauni milioni 19 kwa mwaka.

Mchezaji mwingine ambaye anatarajia kuongoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani badala ya Tevez atakuwa kiungo wa klabu ya Chelsea, Oscar dos Santos, ambaye atachukua kitita cha pauni 400,000 kwa wiki, huku kwa mwaka akichukua pauni milioni 20.8 endapo atakamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Shanghai SIPG ya nchini China.

Kwa upande wa Tevez, mwenye umri wa miaka 32, tayari amewaaga mashabiki wake wa klabu ya Boca Juniors mara baada ya kucheza mchezo wa juzi dhidi ya Colon, huku klabu yake ikishinda mabao 4-1, yeye akifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya West Ham, Manchester United, Manchester City na Juventus, aligusa hisia za mashabiki wengi ambao walijitokeza kwenye uwanja huo, huku wakionekana kuwa na mabango ambayo yanaonesha kuthamini mchango wake na wengine wakimtaka aendelee kuitumikia timu hiyo kwa miaka ijayo.

Kuna shabiki mmoja alionekana kuingia uwanjani huku akilia kwa furaha na kumpigia magoti mchezaji huyo na kumpongeza kwa kile ambacho amekifanya tangu kujiunga kwake kwa mara ya pili mwaka 2015.

Wachezaji wengine ambao wanaongoza kwa kulipwa fedha nyingi duniani mbali na Messi na Ronaldo ni Gareth Bale, ndani ya klabu ya Real Madrid ambapo anachukua pauni 346,000 kwa wiki, huku akichukua pauni milioni 18 kwa mwaka. Givanildo de Sousa ‘Hulk’ ambaye anakipiga katika klabu ya Shanghai SIPG, anachukua pauni 317,000 kwa wiki, huku kwa mwaka akichukua pauni milioni 16.5, akifuatiwa na Paul Pogba wa Man United ambaye anachukua pauni 290,000 kwa wiki, huku kwa mwaka akichukua pauni milioni 15, na Neymar, ambaye anachukua pauni 289,000 kwa wiki na kwa mwaka akichukua pauni milioni 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles