23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MSD YAKARIBISHA UWEKEZAJI VIWANDA VYA DAWA NCHINI

Duka la dawa jumuiya Mhumbili
Duka la dawa jumuiya Mhumbili

Na ESTHER MNYIKA – DAR ES SALAAM

KUJENGWA kwa viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini  kutasaidia kutatua changamoto ya kukosekana kwa dawa hospitalini na kuleta ufanisi wa upatikanaji kwa  Watanzania.

Katika kuelekea Tanzania ya viwanda, Bohari Kuu  ya Dawa (MSD) ipo kwenye mchakato wa kuanzisha viwanda vya kuzalishia dawa na vifaa tiba nchini kupitia mpango wa ushirikiano na sekta binafsi katika ubia.

Kujengwa kwa  viwanda vya kuzalisha  dawa  na vifaa tiba nchini  kutapunguza gharama  za kuagiza  dawa nje ya nchi kama ilivyo kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo ya kuendeleza  viwanda, MSD ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha upatikanaji wa kiwanja chenye ekari 100 katika eneo la Misugusugu, Wilaya ya Kibaha mkoani  Pwani  kwa ajili  ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu, anasema bohari hiyo  imeanzisha mchakato wa kujenga viwanda  hivyo nchini kupitia  mpango wa ushirikishwaji  wa  sekta binafsi.

Anasema dawa na vifaa tiba  vinavyotegemewa  kuanza kuzalishwa  katika awamu ya kwanza  ni pamoja na IV fluids, Syrups, Cotton Wools na Surgical gloves.

Anasema kwa mda mrefu MSD katika Kanda ya Dar es Salaam, imekuwa inakabiliwa na ufinyu wa eneo la kuhifadhia dawa na vifaa tiba, hivyo kulazimu  kukodi maghala  ambayo yamekuwa  yakiigharimu MSD takribani Sh bilioni 4 kwa mwaka.

Anasema  kutokana na hali hiyo, Rais Dk. John Magufuli  aliahidi  kutoa eneo  kwa ajili ya kuepuka gharama hizo  na baada ya  ahadi hiyo  Machi mwaka jana, Waziri wa Ardhi na Mendeleo ya Makazi, William Lukuvi, aliikabidhi MSD hati ya kiwanja  cha ukubwa wa ekari tano kilichopo eneo la Luguruni Wilaya ya Ubungo, kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa maghala na ofisi.

Anasema hata hivyo MSD itaendelea  kukaribisha wawekezaji  wanaotaka kuongeza wigo  wa uzalishaji  kulingana   na uwezo wao wa kifedha na kiteknolojia.

“Sisi kama MSD tunatoa ardhi na soko kwa wawekezaji ila ni lazima  utengeneze dawa na vifaa tiba  vyenye viwango  na ubora  ili kupata soko kwa urahisi kwa wateja  kutokana  na bidhaa kuwa nzuri,” anasema Bwanakunu.

Anasema watu binafsi na wadau  wanatakiwa kufungua  viwanda vingi  vya  dawa  ili  kupunguza kuagiza dawa nje ya nchi.

Bwanakunu anasema MSD wameanza  utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba  moja kwa moja kutoka  kwa wazalishaji na kuhakikisha  kuna upatikanaji endelevu na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa  hizo ambazo asilimia 80 zinatoka nje ya nchi.

Anasema utaratibu huo   utasaidia kupunguza  gharama za ununuzi wa dawa na vifaa kutoka kwa wafanyabiashara.

“ Hata hivyo, MSD hadi sasa   imeshatoa  mikataba 58 ya ununuzi wa dawa muhimu  mbalimbali kutoka kwa wazalishaji wa ndani na nje ya nchi na wanatafuta  wazalishaji 78  wa dawa na wazalishaji 76 ni wa vifaa tiba,” anasema.

Anasema kwa sasa wanahitaji kuhamasisha wawekezaji  kwa sababu wana faida nyingi iwapo mitaji yao itakua na manufaa.

Anasema katika  kuhakikisha inaongeza ufanisi  katika shughuli za upokeaji , utunzaji na usambazaji   wa dawa na vifaa tiba, MSD imeendelea  kuboresha mfumo wa  msimbo pau ‘barcode’.

Anasema mfumo huo  ni wa kisasa utakaosaidia katika shughuli za ugavi wa dawa na vifaa tiba.

Anasema MSD wameanzisha  mpango wa huduma maalumu  kwa wateja wake wakubwa  wenye lengo la kuwawezesha wateja hao  kupata huduma kwa haraka  zaidi  pindi wanapokuwa  wanahitaji dawa.

Bwanakunu alitaja baadhi ya wateja hao kuwa  ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Mirembe, Hospitali ya Kanda ya Mbeya, KCMC, Hospitali ya Amana, Temeke, Mwananyamala, Mnazi Mmoja na nynginezo.

Aidha, anasema  ndani ya mwaka jana MSD ilifanikiwa kufungua maduka saba  ya dawa sehemu mbalimbali nchini.

Anasema lengo la kufungua maduka hayo   ni  kuziwesha hospitali ambazo ndio wateja wakubwa wa kununua dawa kwa ajili ya  hospitali.

Anasema maduka ambayo hadi sasa yamefunguliwa  ni pamoja na liliopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sekou Toure (Mwanza), Rufaa Mbeya na nyinginezo.

Bwanakunu anasema katika kipindi cha nyuma, kulikuwa na tatizo la ufinyu wa bajeti lakini kwa sasa hakuna tena changamoto hiyo.

“Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016\17 ilikuwa Sh bilioni 29, ambapo kila mwezi ninapewa Sh bilioni 2  kwa ajili ya kununua dawa na katika  bajeti ya mwaka wa fedha  ijayo  ni Sh bilioni 251 na kila mwezi nitapewa Sh bilioni 21.8,” anasema.

Anasema wanasambaza dawa nchi nzima   na wanatumia Sh bilioni 3 kwa mwaka  na wana magari 100 kwa ajili ya kazi hiyo.

Anasema  Serikali imetenga bajeti kubwa  yenye kukidhi  kasi ya  uingizaji dawa nchini, hadi kufikia  mwishoni mwa mwaka jana  hali ya upatikanaji wa dawa  nchini ilikuwa wa kuridhisha.

“Hadi  kufikia mwishoni wa mwezi huu,  aina 17 za dawa  zitawasili na hali itatengemaa kwa asilimia  86, Februari mwaka huu aina tatu za dawa zitawasili  hivyo kuboresha upatikanaji wa dawa kwa asilimia 88.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles