23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Msando adaiwa kufanya uchochezi dhidi ya serikali, corona, bado ashikiliwa na polisi

Janeth Mushi, Arusha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linawashikilia watu wawili akiwamo Wakili wa kujitegemea, Albert Msando kwa tuhuma za kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya serikali na kuzungumzia taarifa za ugonjwa corona wakati hana mamlaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 29, mjini hapa, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Koka Moita amesema Msando anashikiliwa kwa mahojiano kuanzia jana.

“Tunamshikilia kwa mahojiano kutokana na  kipande cha video (video clip) iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Msando anaeleza kuwa hali ni mbaya sana Arusha juu ya ugonjwa huo wakati hana mamlaka ya kueleza lolote juu ya ugonjwa huo.

“Msando ametoa kauli hizo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Arusha wakati akigawa vifaa vya kujikinga na virusi vya corona,” amesema.

Aidha, amemtaja mtuhumiwa wa pili kuwa ni Agness Shinji ambaye anadaiwa kusambaza taarifa za uongo mtandaoni ambapo Aprili 9 mwaka huu kupitia group la whatsapp alituma taarifa kwamba mtangazaji wa TBC 1 Gloria Maiko, amefariki kutokana na ugonjwa wa corona kitu ambacho si kweli.

Amesema watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na kutoa onyo kwa makundi yote wakiwamo viongozi wa siasa pamoja na wananchi kutokuwa wasemaji wa serikali na wanapaswa kutii amri na maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles