31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Msamaha kumpeleka Pistorius Olimpiki 2020

Oscar Pistorius
Oscar Pistorius

ADAM MKWEPU NA MITANDAO,

BINGWA wa mbio za Olimpiki za walemavu, Oscar Pistorius, anaweza kuwa miongoni mwa wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki, Tokyo, nchini Japan kama akiomba msamaha kwa jamii ili kuwa sehemu ya mashindano hayo.

Mahakama ya nchini Afrika Kusini ilimhukumu kifungo cha miaka sita jela kwa kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, mwaka 2013 kwa kumpiga  risasi nne.

Hukumu hiyo kwa Pistorius ni mara ya pili baada ya awali kufungwa kifungo cha mwaka mmoja nje kabla ya baadhi ya majaji kugomea uamuzi huo na kutaka kusikilizwa kesi yake.

Jaji wa kesi hiyo, Thokozile Masipa, alimpa Pistorius nafasi ya upendeleo na kuwajibika kwa hukumu ya mauaji kwa kifungo cha miaka sita badala ya miaka 15 kutokana na mazingira ya mwanariadha huyo.

Miaka 15 ni adhabu ndogo ikilinganishwa na kitendo cha mauaji chini ya sheria ya Afrika Kusini, isipokuwa hakimu anaweza kufanya hivyo baada ya Jaji kujiridhisha, huenda yanaweza kuwa mazingira ya kutuliza baada ya awali kuhalalisha adhabu ndogo.

Jaji Masipa anasema  kwamba,  hakukuwa na sababu ya mwanariadha huyo awali kupewa  adhabu nyepesi ambapo ilisababisha majuto.

Kimsingi kesi hiyo ilikuwa na mazingira ya kipekee  kutokana na kitendo cha mauaji na  kuwa miongoni mwa kesi  ya kipekee  kwa kuwa hayakuwa maisha ya kawaida yanayoweza kuhusisha kitendo alichokifanya mwanariadha huyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi  Mkuu wa michuano ya Olimpiki nchini Afrika Kusini, Tubby Reddy, anasema kwamba mwanariadha huyo anaweza kutumikia mwaka mmoja tu akiwa jela na baadaye  kutoka na kuendelea na mazoezi ya kujifua na michuanoa hiyo.

Reddy anasema kwamba hakutakuwa na tatizo kwa mwanariadha huyo kurejea kwenye kikosi cha wanariadha watakaokwenda Tokyo kwa ajili ya  kuliwakilisha taifa lake kwenye michuano hiyo.

Anasema kwamba, mwanariadha huyo anatakiwa kurudi na kuomba radhi kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuishi maisha ya kawaida kama raia mwingine ndani ya Afrika Kusini na kudai kuwa hakuna sheria inayomzuia mwanariadha huyo kujumuika na jamii yake.

Pistorius anatakiwa kufanya hivyo kutokana na kuigawa jamii ndani ya Afrika Kusini kwa kuwa wapo ambao hawatafurahi kwa kitendo cha yeye kuwa huru lakini wengine watakuwa na furaha.

Reddy anasema kwamba, Pistorius anaweza kutumikia kifungo cha nje baada ya mwaka mmoja kuwa jela na kuwa na muda mrefu wa kujiandaa kabla ya michuano hiyo.

Siku ya pili wakati Pistorius akiwa jela na kuelekea hospitali ya Magereza ya  Kgosi Mampuru 11,  walionekana baadhi ya watu kuwa na hisia za hasira juu yake kama vile hawakuwa tayari kumsamehe.

Kesi ya Pistorius ni kama vile ilikuwa vita kwa jamii inayomkubali kutokana na ubora wake  na juhudi katika taifa lake  na wengine ambao hawamkubali kutokana na kitendo alichokifanya juu ya mwanamke asiyekuwa na hatia.

Wapo ambao wanalifananisha tukio hilo na ushindani wa gari la kifahari dhidi ya mwanamke mzuri au kurusha silaha kwa kiumbe kisicho na hatia.

Kilichombana Pistorius ni mfumo wa sheria kwa kuwa inawajibika kutokana na matendo, hivyo  ingawa kesi hiyo kuhukumiwa kutokana na mazingira.

Hata hivyo, ilikuwa vigumu kumuachia mwanariadha huyo aliyethubutu kumuua  mpenzi wake kwa kumpiga risasi nne kupitia mlango wa bafuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles