30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Msako mkali wateja NHC waja

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula amekutana na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa saa nne na kuitaka kuhakikisha kufikia Januari, 2020 inawachukulia hatua wapangaji wote wa Shirika hilo wanaodaiwa kodi inayofikia bilioni 8.23.

Dk. Mabula alikutana na menejimenti  hiyo mwishoni mwa wiki,Dar es salaam ikiwa ni mkakati wake wa kulifanya shirika kuimarika kimapato na kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Alisema katika kuifanya shirikala kuimarika kimapato, lazima madeni kutoka kwa wapangaji wake yakusanywe kwa kuanzisha opreresheni maalumu.

‘’Ukiacha zile taasisi za Serikali, wote wanaodaiwa ikifika Januari, mwakaniwafikishwe kwenye vyombo vya sheria,zile taasisi za Serikali mkamuone Katibu Mkuu HAZINA ili taasisi hizo zikatwe fedha moja kwa moja,’’ alisema.

Alisema wakati wa opresheni ya kukusanya madeni, sheria lazima zifuatwe, ikiwamo kutoa hati za wito wa madai kwa wadaiwa wote kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Mkurugenzi wa Umiliki na Uendelezaji wa NHC, Greyson Godfrey alisema pamoja na kuimarika katika makusanyo, liko kwenye mikakati maalumu wa kukusanya madeni kutoka kwa wadaiwa wake na moja ya jitihada zake ni kuingia makubaliano maalumu ya namna wadaiwa watakavyolipa madeni.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk.Maulid Banyani alisema shirika limekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha linaimarika kimapato.

Alisema linatoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri katika mikoa itakayofikia lengo la makusanyo.

‘’Tumekuwa tukitoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri na sasa tunaangalia ile mikao ambayo haina malimbikizo ya madeni kwa wapangaji wake kwa asilimia mia moja tuone namna tutakavyotoa motisha ili kuhamasisha mikoa kutokuwa na madeni,’’ alisema.

Alisema limeanza kufanya uhakiki kwa wapangaji wake ili kubaini wapangaji waliopangisha watu wengine ambapo eneo la Ubungo limetumika kama eneo la majaribio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles