27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MREMA, LISSU WAPIGANA VIJEMBE

Na KAMILI MMBANDO (TSJ)-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Akizunguma na MTANZANIA kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia  mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.

“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.

Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.

Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.

“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.

Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba                                                                                                                                                                                                                       wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles