Mpinzani wa Kagame, mama yake waachiwa huru kwa dhamana

0
615

Kigali, Rwanda

Hatimaye Mahakama Kuu mjini Kigali, imemuachilia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, na mama yake ambapo watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza.

Jaji wa hiyo, amesema maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi pasipoti zao kwa mwendesha mashitaka na wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali, bila kibali maalumu.

Rigwara, alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara, Septemba mwaka jana nyumbani kwake mjini Kigali, Rwanda.

Wawili hao walikuwa kizuizini kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Lakini walikanusha madai hayo na kusema yana misingi ya kisiasa.

Rwigara, hakufanikiwa kuwania uraisi na alipigwa marufuku baada ya uchunguzi kubaini kuwa alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono kugombea kwake.

Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapinduzi ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here