30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MPINA AITAKA TGTS KUONDOKA KABLA YA JANUARI 2018

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameutaka uongozi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris (TGTS),  kuangalia na kupitia nyaraka zao kama zina uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu  tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na  Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO) kabla ya serikali haijawaondoa kwa nguvu Januari mwakani.

Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa, Desemba 8, alipotembelea Ranchi ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali katika Ranchi hiyo ambapo amemtaka mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo endapo atabaini kuwa amekuwa akikaa kimakosa kuanzia katika  vitalu namba 41 hadi 49.

Aidha Waziri Mpina amesema endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki baada ya muda huo, Serikali itamuondoa kwa nguvu  na atatakiwa kulipa gharama  zote za fidia na usumbufu.

“Ninakuagiza angalia taarifa ulizonazo kuhusu umiliki wa eneo hili kama utaona umeendelea kukaa hapa bila kufuata taratibu tafadhali uondoke mara mmoja ili kupisha Serikali kuendelea na shughuli zake,” amesema Mpina.

Pia Mpina  amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa Philemoni Wambura kuwaandikia barua  ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40 na ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia 40 wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari Mosi mwakani.

Mpina amewaonya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wana uwezo wa kuwekeza katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa kwani amegundua baadhi ya ya wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani  na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.

Hata hivyo, awali Meneja wa TGTS, Audax Kalulama akizungumza kwa simu na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema eneo hilo wanamiliki kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na Wizara ya Mifugo kuonyesha taarifa  za umiliki wa eneo hilo.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles