25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mpango wa Trump kuigawa Israel, Palestina waingia shubiri

Gaza, Palestina

WAPALESTINA wamepuuzilia mbali mpango mpya wa Rais wa Marekani, Donald Trump  kuisuka upya mipaka ili kuleta amani kati yake na Israel, wakitaja kuwa njama.

Mpango huo unapuuza taifa la Palestina na kutambua mamlaka ya Israel kuhusu makaazi yake katika eneo la ukingo wa magharibi.

Chini ya mpango huo, Jerusalem itasalia kuwa mji mkuu wa Israel bila pingamizi, lakini mji mkuu wa Palestina utajumuisha maeneo ya Jerusalem mashariki.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas  tayari amepinga hilo akisema “Jerusalem haitauzwa, haki zetu haziuzwi na wala sio ya kuamua itauzwa kwa fedha kiasi gani ,” aliongeza.

Maelfu ya Wapalestina walifanya maandamano katika ukanda wa Gaza, huku majeshi ya Israel yakipelekwa kulinda maeneo yanayokaliwa na raia wake katika eneo la ukingo wa magharibi.

Mapendekezo hayo ambayo, yanalenga kusuluhisha mzozo wa muda mrefu duniani, yalitayarishwa chini ya usimamizi mume wa binti ya Trump, Jared Kushner.

Ripoti zinasema Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anapanga kushinikiza baraza la mawaziri kupiga kura ya kuidhinisha 30% ya makazi yake katika eneo la ukingo wa Magharibi katika kikao kitakachofanyika siku ya Jumapili.

Israel iliwapeleka karibu wayahudi 400,000 katika makaazi ya Wapalestina yaliyopo ukingo wa magharinbi huku wengine 200,000 wakiishi mashariki mwa mji wa Jerusalem.

Makazi hayo yanachukuliwa kuwa kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, japo inapinga hili.

Katika tamko lake la siku ya Jumanne Mahmoud, alisema haiwezekani hakuna Mpalestina, mwarabu, Muislamu au mtoto wa Kikristo atakayekubali taifa la Palestina bila Jerusalem kuwa mji wake mkuu.

“Tunasema La, La ,La mara elfu moja,” alisema  na kuongeza; “Tumepinga mpango huu kuanzia mwanzo na msimamo wetu uko sawa.”

Wanamgambo wa Kipalestina ambao ni kundi la Hamas linalodhibiti ukanda wa Gaza pia limepinga mpango huo likiongeza kuwa ni njama ya “kusambaratisha miradi ya kitaifa ya Palestina”.

Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha mpango kazi kuhusu Mataifa ya mashariki ya kati ambao ulikwa ukisubiriwa kwa muda mrefu, ukiahidi kuwa Jerusalem utabaki kuwa mji mkuu wa Israel.

Umoja wa Mataifa umesema utajitolea kusuluhisha mzozo wa mpaka baina ya mataifa hayo mawili  kabla ya mapigano ya mwaka 1967, wakati Israel iliponyakua eneo la wa magharibi na Gaza.

ALICHOKISEMA NETANYAHU

Kwa upande wake Netanyahu alielezea mpango wa Trump kama” Mpango wa karne…Israel haitapoteza hii fursa “.

“Mpla atubariki sote kwa usalama,maisha marefu na amani!” aliongeza.

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres alitoa wito wa kufikiwa kwa mkataba wa amani kwa kuzingatia azimio la Umoja wa mataifa, sheria ya kimataifa na makubaliano ya pande mbili.

Kutokana na hayo, Jumiya ya mataifa ya Uarabuni imesema itafanya kikao cha dharura siku ya Jumamosi kujadili suala hilo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab ametoa wito kwa Palestina kutathmini mpango huo  pasipo kuegemea upande wowote kama hatua ya kwanza kuelekea mashauriano  yatakayofikia suluhisho la kudumu.”

“Leo Israel inapiga hatua kubwa ya amani,” Trump aliwaambia maofisa na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani.

“Dira yangu ni kuwasilisha fursa ya ushindi katika pande zote mbili, ili kutatua mgogoro huu unaouweka Palestina katika hatari ya kutokuwa taifa huru dhidi ya vikosi vya usalama vya Israel.”

YALIYOPENDEKEZWA

Marekani itatambua mamlaka ya Israel katika himaya ambayo iko kwenye mpango wa Trump kuwa ni sehemu ya Israel.

Ramani iliyoandaliwa na Trump imeongeza himaya ya Palestina kuwa mara mbili na mji mkuu wa Palestina kuwa mashariki ya Jerusalem.

Jerusalem utabaki kuwa mji mkuu ambao haugawanyiki.

Taasisi ya Palestina inayofahamika kama’ Palestine Liberation Organisation (PLO)’ ilisema kuwa mpango wa Trump ulipaswa kuipa Palestina zaidi ya asilimia 15 ya sehemu ya kihistoria ya Palestina.

“Si mpalestina wala muisraeli ataondolewa katika makazi anayoishi kwa sasa” – mpango huo umependekeza kuwa himaya ya wayahudi wa Israel itaendelea kubaki eneo la ukingo wa magharibi.

Vilevile alibainisha kuwa ukingo wa magharibi hautagawanywa nusu kwa nusu katika mpango huo.

“Tutatengeza mipaka ya himaya hiyo katika siku za baadae katika taifa la wapalestina, wakati ambao taifa limefikia makubaliano na kujiondoa katika ugaidi”, alisema Trump.

Israel watafanya kazi na mfalme wa Jordan kuhakikisha kuwa eneo la takatifu la Jerusalem linalojulikana kama makazi ya wayahudi na kunatunzwa na waislamu pia.

Himaya iliyoelezwa na Trump kuwa ya wapalestina katika ramani, inaonyesha kuwa eneo hilo litabaki kuwa wazi na kutoendelezwa kwa chochote kwa muda wa miaka minne.

“Wapalestina wanaishi katika umaskini na ghasia, wanakabiliwa na ugaidi na hawana maisha bora. Wanapaswa kuwa na maisha bora sasa”, alisema Trump.

Akiwa amesimama pamoja na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema kuwa hii ni fursa ya mwisho kwa Wapalestina.

Trump pia alisema ubalozi wa Marekani utakuwa wa wazi.

Tayari Palestina wamesisitiza kuwa mashariki ya Jerusalem, ilichukuliwa na Israel mwaka 1967 katika vita ya mashariki ya kati hivyo mji huo mkuu unapaswa kuwa wao.

Maofisa wa Israel wanasema kuwa Netanyahu amekwenda Moscow kujadili mapendekezo hayo na rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Amependekeza kuwa taifa huru la Palestina na mamlaka ya Israel inapaswa kulitambua taifa hilo kuwa liko katika makazi ya ukingo wa magharibi.

Mpango huo unaofahamika kama ‘The blueprint’ umelenga kutatua tatizo moja duniani ambalo limekuepo kwa muda mrefu, ni mgogoro wa muda mrefu.

Balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman, alisema kuwa muda ambao wametangaza mabadiliko hayo hawakuhusisha maendeleo yeyote ya kisiasa na kuongeza kuwa mpango huo ulikuwa umekamilika muda kidogo.

Zaidi ya Waisraeli 400,000 ambao wanaishi eneo la ukingo wa magharibi, makazi hayo yanadaiwa kuwa kinyume na sheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ingawa Israel wanapuuzia jambo hilo.

Friedman alisema kuwa Israel haipaswi kusubiri bali wanapaswa kuondoka katika himaya hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles