24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wakimbiza maelfu ya wananchi

MALLACOOTA, Australia

MAELFU ya watu nchini Australia, wamekimbilia ufuo wa bahari kujinusuru na moto wa nyikani ambao unaoelekea maeneo ya pwani.

Wakaazi wa Mallacoota wameuelezea moto huo kuwa “kisa cha kuogofya,” huku wakisimulia jinsi walivyoona anga ilivyobadilika rangi nyekundu wakiwa ndani ya boti.

Maofisa walithibitisha  watu wawili wamefariki dunia kutokana na moto huo katika mji wa New South Wales  kufikia sasa vifo 12, vimehusishwa na janga hilo la moto.

Mamlaka pia zinasema watu wanne hawajulikani waliko katika miji ya Victoria na NSW.

Miili ya waathiriwa wa hivi punde ambayo inaaminiwa ya baba na mwanawe wa kiume ilipatikana katika mji wa Corbargo eneo la NSW, ambalo lilikumbwa na moto siku ya Jumanne.

“Hali ya kusikitisha,” alisema naibu wa kamishena wa polisi katika eneo la NSW Gary Worboys. “(bila shaka), walikuwa wanajaribu kujinusuru kutokana na moto huo kwa sababu ulizuka mapema saa za asubuhi.”

Mjini Mallacoota, wahudumu wa kitengo cha kuzima moto, walisema mkondo wa upepo umebadilika na kuongeza kuwa hali hiyo imegeuza mkondo wa moto kutoka maeneo ya makazi.

Maeneo kadhaa ya kujivinjari msimu wa sherehe katika mwambao wa pwani kati ya miji ya Sydney na Melbourne kwa sasa yamekatizwa kutokana na moto huo.

Gavana wa Jimbo la Victoria, Daniel Andrews alisema meli huenda zikatumwa kuwapelekea waathirika wa moto huo chakula, maji na nguvu za umeme maeneo hayo.

“Baadhi ya watu waliotengwa wanaweza kufikiwa kupitia bahari,”alisema.

Mamlaka zilitoa wito kwa watu wa eneo hilo wengi wao watalii kutoondoka, lakini ilipofika Jumatatu hali ilikuwa mbaya na hatari kufanya shughuli ya kuwahamisha.

Moto wa nyikani  eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, imetokana na ongezeko la viwango vya joto, upepo mkali na radi ya wakati wa ukame.

Mamlaka pia zinasema zimeripoti kwa watu saba hawajulikani waliko katika eneo hilo wanne kutoka Victoria na watatu wa New South Wales.

“Tunahofia usalama wao. Wamekuwa katika mazingira ya moto,hatuwezi kubainisha waliko sasa,” alisema Waziri Mkuu wa Victoria, Daniel Andrews.

Wakaazi wameiambia BBC, hali ilikuwa ya ”kuogopesha” huku majivu yaliyotokana na moto huo, yakianguka katika fukwe za bahari.

Mji wa Mallacoota, umeathiriwa zaidi na moto huo, na wakaazi walilazimika kukimbilia usalama wao

“Ilikuwa mchana, kulikuwa na giza sawa na usiku wa manane na kile tulichosikia ni sauti ya moto mkali uliokuwa usambaa kwa kasi ya ajabu,” alisema David Jeffrey, mmoja wa wafanyibiashara. “Sote tunahofia usalama wetu.”

Moto huo umeharibu majengo kadhaa, lakini ulikatiza makali yake baada ya mkondo wa upepo katika ufuo wa bahari kubadilika.

Mada zinazohusiana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles