29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wa Amazon wagonganisha vichwa wakuu duniani

BRASILIA, BRAZIL

RAIS wa Brazil, Jair Bolsonaro amepingana na ushauri unaotolewa na mataifa mbalimbali kutokana na hofu ya msururu wa matukio ya moto kwenye msitu wa Amazon.

Kitisho hicho kinatokana na msitu huo unaotajwa kama “mapafu ya dunia”, kuharibiwa na mfululizo wa visa vya moto na kuchochea mjadala mkali kuhusu nani wa kulaumiwa.

Rais Bolsonaro ameandika kwenye ukurasa wa twitter kwamba serikali yake imefungua milango ya majadiliano, lakini kwa kuzingatia data halisi na pande zote kuheshimiana.

Rais wa ufaransa Emmanuel Macron aliuita moto huo “janga la kimataifa”, huku akitoa wito kwa wakuu wa mataifa yaliyoinukia kiviwanda duniani, G-7 kufanya kikao cha dharura kujadili janga hilo katika mkutano wao wa kilele unaofanyika Ufaransa, mwishoni mwa wiki hii.”

Aliandika, “nyumba yetu inaungua. Kwa kweli, msitu wa Amazon, mapafu yanayozalisha asilimia 20 ya hewa ya Oksijeni unateketea.”

Bolsonaro alijibu kwa kuandika “Ninajuta kwamba Macron anataka kujiimarisha kisiasa kwa kutumia suala hili la Brazil na mataifa mengine ya Amazoni. Mawazo yake ni ya kikoloni kwa kuyataka mataifa ya G-7 kujadili suala hilo bila ya kushirikisha mataifa mengine ya ukanda huo”.

Msitu wa Amazon umeungua takriba mara 73,000 tangu Januari hadi Agosti mwaka huu Bolsonaro anatoa matamshi hayo wakati Brazil ikiwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira utakaofanyika mjini Salvador, kuelekea mkutano wa kilele nchini Chile, mwezi Disemba.

Jamii ya watu wanaoishi kwenye msitu huo wameeleza kusikitishwa kwao na namna msitu huo unavyoteketezwa.

Handech Wakana Mura ni kiongozi wa jamii hiyo ambaye anasema  “Tunasikitika kwa sababu msitu huu unateketea kila wakati, tunahisi hali ya hewa inabadilika na dunia inauhitaji huu msitu. Tunauhitaji pia na watoto wetu wanauhitaji,”.

Wataalamu wa mazingira wanasema uharibifu kwenye msitu huo ulioongezeka kwa mara tatu ilipofika mwezi Julai ikilinganishwa na mwaka jana.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake mkubwa kutokana na moto kwenye msitu huo.

Aliandika kwenye twitter, “katika wakati ambapo kuna mzozo mkubwa wa hali ya hewa, hatuwezi kubeba mzigo mwingine wa uharibifu wa chanzo kikuu cha Oksijeni na bayonuwai. Ni lazima Amazon ilindwe”.

Mapema, mkuu wa utumishi wa rais Bolsonaro, Onyx Lorenzoni aliyatuhumu mataifa ya Ulaya kwa kuongezea chumvi changamoto za kimazingira nchini Brazil ili kuvuruga maslahi yake ya kibiashara.

Takwimu rasmi zinaonyesha visa 73,000 vya moto viliripotiwa nchini Brazil katika kipindi cha miezi minane, ikiwa ni idadi ya juu kabisa tangu mwaka 2013.

Nchi jirani, Peru ambayo pia ina eneo kubwa la Amazon imetangaza kujiandaa kupambana na moto huo unaosambaa kwa kasi kutokea Brazil na Bolivia, Paraguay na Bolivia.

Wanapambana kuutenganisha moto huo ambao umeteketeza eneo kubwa la msitu huo ambao ni chanzo cha mvua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles