24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Moshi kinara wa usafi 2019

SAFINA SARWATT -MOSHI 

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, imekuwa mshindi wa kwanza kundi la halmashauri za majiji na manispaa katika Mashindano ya Afya na usafi wa mazingira mwaka 2019.

Akizungumzia ushindi huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi alisema kuwa ushindi huo unatokana na ushirikishwaji wa wananchi katika suala la usafi pamoja na upatikanaji wa vifaa vya usafi. 

Alisema  kuwa, wananchi wa mji wa Moshi wamekuwa na desturi ya kupenda usafi na kwamba wanajivunia kuwa mshindi wa kwanza na kupewa nishani, cheti, ngao na hundi ya Sh million 20.

Mwandezi alisema kuwa, Halmashauri ya Manispaa Moshi kwa sasa inajiandaa kwa Mashindano ya usafi ya mwaka 2020.

“Mwaka huu tunajivunia kuwa nafasi ya kwanza kitaifa kama tunavyojua, Manispaa yetu ya Moshi imekuwa namba moja kwa usafi wa mazingira kitaifa kwa miaka saba mfululizo, isipokuwa mwaka jana ambapo tulishuka kidogo na kushika nafasi ya tatu,” alisema Mwandezi. 

Alisema kuwa, ushindi huo unatokana na Manispaa kuwa na dapo la kisasa la kutupitia taka na kuongeza magari matatu ya kuzoa taka katika ya mji Moshi na maeneo ya pembezoni mwa mji. 

Alisema halmashauri hiyo itaendelea kuboresha suala la usafi na utunzaji wa mazingira .

“Ununuzi wa magari haya ni juhudi za kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika jitihada za kuhakikisha mji wa Manispaa ya Moshi unaendelea kuwa msafi siku zote, pamoja na kupambana na magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles