26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Molde yakubali kumwachia Solskjaer Man United

MANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Molde ya Ligi Kuu Norway  imemtaka kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, abaki  England kuendelea kuifundisha timu hiyo, baada ya mafanikio  aliyoyapata tangu ateuliwe kurithi mikoba ya Kocha Jose Mourinho.

Uamuzi huo unatokana na Solskjaer, kuwa msaada  tangu  atue Manchester United, ambapo  amefikisha michezo nane  bila kufungwa.

Mashabiki wa kocha huyo ambaye aliwahi kuichezea Manchester United kwa mafanikio wamekuwa na raha tangu kufukuzwa  kwa Mourinho Desemba mwaka jana.

Molde  ilikubali kumtoa kwa mkopo   kocha huyo wakiwa katika  mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Norway msimu huu, lakini inadaiwa kuwa wanaweza kumwachia moja kwa moja kutokana na mafanikio anayopata  akiwa Manchester United.

“Nilimpigia simu mmiliki wa Molde, alinieleza Manchester United inanihitaji na ukweli ni kwamba anafahamu hii ndiyo ndoto yangu, alisema: ‘Endelea kuwa  na furaha tafadhali usirudi!
“Viongozi wote wananitakia  kheri hapa United,  wanatambua hapa ndio nyumbani, kama nitarudi pia  Molde nitafanya mambo makubwa nikiwa huko lakini itategemea,” alisema Solskjaer.

Solskjaer alikishuhudia kikosi chake kikifikisha michezo nane bila kufungwa baada ya kupata sare ya kufungana mabao 2-2 na Burnley.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles