25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Moja Bet yapiga hodi Mbeya na Boom Pesa

 

Mwandishi Wetu



Kampuni ya Michezo ya Kubahahatisha ya Moja Bet, imeutambulisha mchezo mpya wa kubahatisha wa Boom Pesa jijini Mbeya unaofahamika kwa kupata washindi kadhaa katika mchezo huo.

Akizungumza jijini Mbeya leo wakati wa uzinduzi wa mchezo huo, Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja kutoka Moja Beti, Florida Mwangosi, amesema mchezo huo ni mpya lakini na ni rahisi kupata fedha tofauti na michezo mingine.

“Huu mchezo wetu wa kubahatisha unaofahamika kwa jina la Boom Pesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake ambapo mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia Sh 100 na kuendelea,” amesema Florida.

Naye Balozi wa  Boom Pesa, Sabrina Ibrahimu,  amesema mwitikio kwa wakazi wa jiji la Mbeya kwenye mchezo huo wa kubahatisha ni mkubwa  na kwamba wananchi zaidi ya 100 kwa siku moja walijitokeza na kushiriki mchezo huo.

“ Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuupokea huu mchezo wetu mpya wa kubahatisha , nawapongeza sana maana wamekuja na baadhi wameshinda tunawashukuru sana tunawaomba waendelee kuucheza mchezo huu” Alisema Sabrinma Ibrahimu

Aidha baadhi ya washindi wa Boom Pesa kutoka Jijini Mbeya, Yasinta Ndesabula na Tyson John,  wamesema hawakutegemea kushinda katika mchezo huo ambapo wamewahimiza Watanzania wengine kucheza ili waweze kujishindia fedha taslimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles