27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mnangagwa arejea nyumbani hali si shwari

Harare, Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, amerejea nchini kwake baada ya kuvunja ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo, amekamatwa.

Hapo jana Mahakama Kuu mjini Harare ilitoa uamuzi kuwa waziri wa serikali hana haki ya kuagiza kufungwa kwa mawasiliano ya mtandao (internet).

Serikali ya Zimbabwe, imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change, Nelson Chamisa, amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

Makundi ya haki za binadamu yanasema watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitishwa.

Mwenyekiti wa kitaifa wa MDC Tabitha Khumalo, amesema amejificha baada ya polisi na jeshi kuzuka nyumbani kwake usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles