23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA MKOA ANUSURIKA KIFO, WAWILI WAJERUHIWA

Wananchi wakimtazama askari aliyefahamika kwa jina moja la Antony aliyegongwa gari jana asubuhi wakati akimwokoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, asigongwe wakati akiwa katika eneo la lango kuu la Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wakati wakielekea Uwanja wa Samora kwenye mazoezi. Watu wawili walijeruhiwa.
NA FRANCIS GODWIN -IRINGA

MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amenusurika kifo, huku askari wawili wakijeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha teksi.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya  saa 12.25 asubuhi eneo la nje ya  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Barabara ya Pawaga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema katika tukio hilo, askari polisi Antony Mwita alijeruhiwa wakati akijitosa kumwokoa Masenza asigongwe na gari hilo dogo aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T 479 CKZ, ambalo liliparamia wananchi waliokuwa katika maandalizi ya kuanza mazoezi ya viungo yaliyofanyika Uwanja wa Samora.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini, Abed Kiponza,  aliyekuwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema kuwa alikuwa hatua kama 15 kutoka  eneo la ajali na aliona gari hilo  likiwavaa watu hao, ambao  walikuwa kando ya barabara.

Kiponza alisema kama si askari huyo kumsukuma kwenye mtaro RC Masenza basi gari hilo lingemgonga.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, aliwataja majeruhi ni askari mwanamke wa Jeshi la Magereza, Greety Mwakipesile ambaye inadaiwa alivunjika mguu na Mwita aliyeumia usoni.

Kwa mujibu wa Kasesela, Masenza yupo salama na alijumuika na wananchi katika mazoezi hadi mwisho.

Aidha Kasesela alimpongeza Mwita aliyefanya jitihada kumwokoa RC Masenza na  askari wengine walioshiriki kumkamata dereva wa gari hilo pasipo kutumia nguvu yoyote na kuwataka wananchi kuiga mfano huo wa ukamataji salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles