‘MKUU WA JESHI  MYANMAR ANAPASWA KUSHITAKIWA’

0
572

GENEVA, USWISI


WACHUNGUZI wa Umoja wa Mataifa jana walitoa mwito ufanyike uchunguzi wa kimataifa na hatimaye kuwafungulia mashitaka maofisa waandamizi wa Jeshi la Myanmar kwa tuhuma za kuhusika na mauaji dhidi ya Waislamu wachache wa jamii ya Rohingya.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesisitiza kuwa Mkuu wa Jeshi, Jenerali Min Aung Hlaing, lazima achunguzwe na hatimaye kushitakiwa kuhusiana na mauaji yaliyofanyika katika jimbo la Rakhine.

Hiyo ni pamoja na mashitaka ya uhalifu wa vita dhidi ya binadamu katika majimbo ya Rakhne, Kachin na Shan.

Warohingya wapatao 700,000 kutoka jimbo la Rakhne walikimbilia Bangladesh baada ya Myanmar kuanzisha operesheni ya ukatili Agosti mwaka jana baada ya  uasi.

Uasi huo uliambatana na matukio ya mauaji, uchomaji moto na ubakaji uliofanywa na wanajeshi katika taifa hilo na wanamgambo wa Budha.

Hata hivyo, Serikali ya Myanmar imekuwa ikikanusha tuhuma hizo na kusisitiza hatua hiyo ilikuwa ni kujibu mashambulio yaliyofanywa na waasi wa jamii ya Rohingya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here