23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano mkubwa ATAPE waanza Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma wajasiriamali wa Kanisa la Wadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), umeanza rasmi leo mkoani Simiyu.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umebainisha mafanikio yaliyofikiwa na chama hicho ikiwamo kupata zaidi ya Sh bilioni moja katika miradi ya maendeleo nchini.

Mkutano huo unaofanyikia katika Shule ya Sekondari Kusekwa iliyoko Mjini Bariadi, zaidi ya wanataaluma na wajasiriamali 1,500 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wameshiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama hicho, Freddie Maneto amesema ATAPE kimewekeza katika miradi ya Afya, Kilimo, Elimu, Maji, pamoja na ujasiriamali.

“Tuna hospitali mbalimbali, shule, mashamba zaidi ya hekari 10,000 ambayo tumelima mihogo, miti na korosho, hivyo tunapoadhimisha miaka 20 ya uwepo wa chama chetu, tunajivunia kuwa miongoni mwa taasisi ambayo imeajiri Watanzania wengi,” amesema Maneto.

Aidha, mwenyekiti huyo amesema katika kutoa huduma kwa wananchi, wanatarajia kuleta mradi wa maji mkoani Simiyu, kutokana na mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wake.

Hata hivyo, wananchi wa mkoani Simiyu wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kuendelea kuwaletea fursa mbalimbali ambapo wanategemea kuongeza kipato kupitia biashara zao.

“Hii ni fursa kubwa kwetu, kama wananchi wa Simiyu, watu zaidi ya 15,000 ni wengi tutaongeza kipato kupitia biashara mbalimbali, kwa sasa katika mji wetu wa Bariadi nyumba za kulala wageni zote zimejaa, watu wamefanya biashara,” amesema John Bubinza mkazi wa Bariadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles