24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MKURUGENZI UBUNGO AJENGA MADARASA YA KISASA SEKONDARI YA URAFIKI

Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John Kayombo amejenga madarasa mawili katika Shule ya Sekondari ya Urafiki iliyopo katika Kata ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Kayombo amesema amefanikisha ujenzi huo kwa kushirikiana na wadau wa elimu ambapo shule hiyo ilianzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Hii ni shule ya mfano, iko katika Kata ya Ubungo karibu na Urafiki Social Hall, ni miongoni mwa Kata 14 za Manispaa ya Ubungo ilianzishwa na Makonda akiwa Mkuu wa Wilaya mimi namalizia kazi tu, ni moja kati ya shule ya mfano, nawakaribisha watu waje wajifunze ujenzi huu,” amesema Kayombo.

Mkandarasi anayesimamia ujenzi huo aliyejitambulisha kama mdau wa elimu amesema madarasa hayo ni ya kisasa ambayo kwa sasa yataezekwa paa kulingana na jinsi mahitaji yatakavyoongezeka, inawezekana kuongeza madarasa mengine juu ikawa ghorofa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles