26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MKUCHIKA: TAARIFA ZA WASTAAFU ZIHAKIKIWE KABLA HAWAJASTAAFU

Leonard Mag’oha, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amewataka maofisa utumishi wa umma nchini, kuhakikisha wanahakiki taarifa za watumishi wanaotarajia kustaafu miezi sita kabla ya muda wa kustaafu.

Mkuchika amesema hayo leo Mei 4, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua programu za shahada za utunzaji kumbukumbu na nyaraka pamoja na uhazili katika Chuo cha Taifa cha Utumishi wa Umma.

Amesema wastaafu wamekuwa wakitumia muda mwingi kufuatilia mafao yao baada ya kustaafu kutokana na uzembe wa maofisa utumishi katika halmashauri mbalimbali na baadaye kuwataka wastaafu hao kufuatilia taarifa hizo wenyewe.

“Sasa anamwachia yule mtumishi kuhangaika kwa hiyo unakuta mtumishi ametoka Mtwara, Mwanza anakuja kufuatilia mafao yake wakati ni kazi ambayo anatakiwa aifanye Ofisa Utumishi.

“Utakuta mtumishi mwingine baada ya miaka miwili au mitatu anakufa bado hajalipwa mafao yake kwa sababu karatasi fulani imekosekana,” amesema Waziri Mkuchika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles