30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

 Miundombinu mibovu kikwazo cha maendeleo Kilolo

                      Raymond Minja, Iringa



Wananchi wa Kata ya Masisiwe wilayani Kilolo wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha uzalishaji wa mazao pamoja na vifo kwa wakina mama wajawazito .

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah alipokuwa akikagua shughuli za maendeleo mmoja wa wakazi wa eneo hilo Iginasi Kanyika amesema miundombinu mibovu ni changamoto hasa kipindi cha mvua na wakazi wa kata hiyo hutegemea kilimo cha mahindi na njegere lakini hali ya kiuchumi imekuwa ikishuka kila kukicha kutokana na kukosa barabara inayowaunganisha hadi makao makuu ya wilaya hiyo.

“Mkuu wa wilaya umekuja tusaidie hii barabara ya nyagiwete maana hata shughuli nyingine za maaendeleo tunashindwa kushiriki sio kuwa hatutaki ila inafika mahali unashindwa peleka mzigo wako sokoni kwenye solo la kuaminika na badala yake tunasubiri walanguzi ndio waje wanunulie hapa”.

Akizungumzia mikakati ya Serikali juu ya kutatua adha hiyo Meneja wa wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA ) Asheri Kajinge, amesema kwa sasa wanachokifanya ni kurekebisha maeneo korofi ili yaweze kupitika kiurahisi kipindi cha mvua na barabara ya kidabaga bomalang’ombe tayari imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na wabasubiria bajeti ili barabara hiyo iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

Naye mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa serikali imedhamiria kuunganisha maeneo yote kwa lami hivyo wananchi hao wasiwe na wasiwasi kwani wataweza kusafirisha mazao yao na kuwawahisha wagonjwa hospitali ya wilaya kwa haraka zaidi.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya ametumia wasaa huo kuwasaa wakazi wa kijiji hicho kuacha kunywa pombe wakati wa kazi na badala yake wachape kazi kwani unywaji wa pombe kupita kiasi hukwamisha maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles