31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MITI YA MATUNDA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

NA SIDI MGUMIA, ALIYEKUWA KIGOMA

UPANUZI wa mashamba unaokwenda sambamba na ukataji wa miti  unahusishwa na matokeo ya  mabadiliko ya tabia nchi.

Hali hii inaleta ukame na ongezeko la joto katika maeneo husika.

Kumekuwa na jitihada nyingi za  kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa  kupanda miti na kutoikata.

Kikundi cha akina mama cha Green Voices Makongoro, Kigoma ni moja ya maundi machache nchini yaliyoamua  kujikita katika mradi wa  ustawishaji wa miti ya matunda.

Wataalamu wanaeleza kuwa miti ya matundi ni njia nyingine ya kuhifadhi mazingira na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mradi huo, Evelyn Kahembe, miti ya matunda  inasaidia  kupunguza hewa ya ukaa, ongezeko la joto, na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua, kuimarisha utunzaji wa maji ardhini.

Kahembe aliongeza kuwa zaidi ya yote, miti ya matunda inasaidia kuongeza uhakika wa chakula na kipato kwa jamii husika.

“Kwa kuwa miti ya matunda itakuwa na thamani kwa familia, si rahisi kukatwa kwa matumizi mengine kama vile kuni au mkaa,” alisema Kahembe

Mwanakikundi Halima Salumu akizungumzia namna wanavyofanya kazi katika mradi wao wa kupanda miti ya matunda, alisema  elimu ya uzalishaji wa miche na utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi.

Chimbuko la kazi hii ni moja ya miradi inaloyenga utekelezaji wa shughuli za mpango mpya unaohusu hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halamshauri ya Kigoma, Minza Edward alisema Mradi huu  unahusika na kulinda mazingira na kuboresha uchumi wa wanawake na kuongeza  kipato.

“Mradi wa Green Voices unafanya vizuri kwasababu kuna kikundi kinafaya kazi huko Mkongoro, wana kitalau na wananufaika kwa kupata matunda, wanakula na kuuza pia na inatunza maingira.

“Kama Halmashauri tunawasapoti kwa upande wetu haswa pale wanapohitaji elimu, huwa tunatuma wataalamu wetu ambao wanawaelimisha, lakini pia watanatoa  mikopo kwa ajili yakuendeleza kile wanachofanya.

“Mradi upo vizuri na tunawashukuru wafadhili wa mradi

“Mikopo tunatoa sio tu kwa wanawake wa Green Voices bali ni kwa wanawake wote na huwa tunatoa kwa vikundi na  kulingana na mahitaji yao.

“Upande wa Mafunzo tunayo idara ya mazingira, tunaitwa pindi wanapotuhitaji.

“Serikali hatutoi ardhi kwa wanavikundi, tunawaacha  wenyewe wanatafuta shamba iwe kwa kununua  au  kukodi.”

Akizungumzia suala la ushirikiano Mratibu wa Green Voices Tanzania, Secelela Balisidya amesema anafurahi kuona ushirikiano uliopo kati ya wana Green Voices Kigoma na Halmashauri.

Alisema  hiyo ndiyo namna pekee ya kuufanya mradi uwe endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles