24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MITI YA MATUNDA ITASAIDIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

 

NA SIDI MGUMIA, ALIYEKUWA KIGOMA

UKATAJI wa miti kwa ajili ya maandalizi ya mashamba unatajwa kuwa moja ya sababu kubwa za mabadiliko ya tabia nchi.

Jambo hili huchangia kuleta ukame na ongezeko la joto kwenye maeneo husika.

Kumekuwa na jitihada kadhaa katika kuihamasisha jamii kuhifadhi mazingira, jamii inaaswa kutokata miti na pia  maelfu ya miti imepandwa.

Miongoni mwa waongoza kampeni hizo ni kikundi cha akina mama cha Green Voices Mkongoro, kilichopo mkoani  Kigoma.

Kikundi hiki kimeamua kujikita katika ustawishaji wa miti ya matunda kama njia nyingine ya kuhifadhi mazingira na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi.

Kulingana na maelezo ya Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Prosper Mtana, miti ya matunda itasaidia kupunguza hewa ya ukaa, ongezeko la joto na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua, kuimarisha utunzaji wa maji ardhini katika maeneo ya mashambani.

Mtana aliongeza kuwa zaidi ya yote, miti ya matunda itasaidia kuongeza uhakika wa chakula na kipato kwa kaya mbalimbali.

“Kwa kuwa miti ya matunda itakuwa na thamani kubwa kwa familia, si rahisi kukatwa kwa matumizi mengine kama vile kuni na mkaa,” alisema Mtana

Mwanakikundi Mariam Abdallah akizungumzia namna wanavyofanya kazi katika mradi wao wa kupanda miti ya matunda, alisema  elimu ya uzalishaji wa miche na utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi.

Chimbuko la kazi hii ni moja ya miradi inaloyenga utekelezaji wa shughuli za mpango mpya unaohusu hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya Kigoma, Minza Edward alisema mradi huo unahusika na kulinda mazingira na kuboresha uchumi wa wanawake.

“Mradi wa Green Voices unafanya vizuri kwasababu kuna kikundi kinafanya kazi huko Mkongoro, wamepanda miti, inawanufaisha, wanapata matunda, wanakula na kuuza, lakini pia wanatunza mazingira.

“Kama Halmashauri tunawasapoti kwa upande wetu hasa pale wanapohitaji elimu, huwa tunatuma wataalamu wetu ambao wanawaelimisha lakini pia kwasababu ni akina mama wanatoa na mikopo kwa ajili yakuendeleza kile wanachofanya.

“Mradi upo vizuri na tunawashukuru wafadhili, mikopo tunatoa kwa wanawake wote waliojiunga kwenye vikundi kulingana na mahitaji yao.

“Upande wa mafunzo tunayo idara ya mazingira, pale wanapotuhitaji tunekwenda kushirikiana nao.

“Hatutoi ardhi kwa mtu mmoja mmoja  ni kwa vikundi, wao wanatafuta shamba iwe kwa kununua au kukodi. Ili wafanyie kazi.

Akizungumzia suala la ushirikiano,  Mratibu wa Green Voices Tanzania, Secelela Balisidya alisema amefurahi kuona ushirikiano uliopo kati ya wana Green Voices Kigoma na Halmashauri kwakua hiyo ndiyo namna pekee ya kuufanya mradi uwe endelevu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles