MISS TANZANIA 2018 AZINDULIWA (CROWN) MPYA YA MILLIONI SITA

0
856

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Kamati ya shindano ya Miss Tanzania imezindua taji jipya (Crown) linalotarajiwa  kuvalishwa mshindi wa shindano hilo atakayepatikana kati ya warembo 20 watakaochuana usiku wa Septemba 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam muaandaji wa shindano hilo, ambae pia ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi amesema taji hilo la mwaka huu linathamani ya Sh milioni sita na lina utofauti na mataji ya miaka iliyopita.

“Taji analotarajiwa kuvishwa mshindi wa mwaka huu lina thamani ya shilingi millioni 6 na lipo tofauti kwa sababu hii ni Miss Tanzania mpya hivyo basi lazima tuwe na vitu vipya,’’ alisema Basila.

Akizungumzia kuhusu zawadi kwa mshindi amesema atapewa gari lenye ubora wa kuendana na hadhi ya mashindano hayo.

“Kwa upande wa zawadi tunayompa mshindi  tumezingatia gari ambayo atapewa  ina ubora kuendana na mashindano na mshindi atapata gari zuri tu,”amesema.

Mashindano haya kwa mwaka huu yanaandaliwa Kampuni mpya ya The Look Company ambayo Mkurugenzi wake ni Basila Mwanukuzi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here