27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mikopo mingi chechefu inatokana na wafanyakazi wa benki wasio waaminifu’


‘Mikopo mingi chechefu inatokana na wafanyakazi wa benki wasio waaminifu’

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amebainisha sababu za benki kutokopesha inatokana na benki zenyewe kutokuwa na wafanyakazi waaminifu kwa kuruhusu wakopaji wasiokidhi vigezo na kusababisha mikopo chechefu.

Kutokana na hali hiyo, amesema BoT imechukua jukumu la kufuatilia kuajiriwa kwa watumishi hao pamoja na mambo mengine.

Profesa Luoga amesema hayo leo Jumatatu Desemba 10, katika mkutano wa Rais John Magufuli na uongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

“Ni kweli benki zinapaswa kuwa huru lakini BoT inapaswa kuangalia mwenendo wao, kwa mfano kuna wakati mikopo ilikuwa haitolewi,BoT imechukua jukumu na imekuwa ikikaa chini na benki nchini kutathmini kwaninimikopo haitolewi na mara nyingi majibu na kwamba benki inaogopa hasara kwasababu watu hawajulikani lakini BoT imechukua jukumu kuhakikisha watuwanajulikana.

“Pia kumekuwa na tatizo la rushwa, wakopaji wengine wabovu wamekuwa wakihonga ili wakopeshwe sasa tunajiuliza inakuwaje benki inamkopesha mkopaji mbovu,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Luoga amesema kumekuwa na tatizo la wafanyakazi wasio na uwezo au ujuzi usiotakiwa kwani si rahisi kuwa benki inakopesha kwa mradi ambao mkopo wake haurudishiki.

“Pale inapoonekana benki haina watu wenye weledi katika uongozi BoT itaendelea kutoa masharti kuwa watu wote lazima wawe na watumishi stahiki,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles