26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mikakati ya China yawatisha Marekani

BEIJING, CHINA

RAIS wa China, Xi Jinping, ametangaza kuwa ni muhimu kwa nchi zaidi duniani kujiunga katika mipango ya mikakati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inayosimamiwa na nchi yake, lakini kwa upande wao bado Marekani imeonyesha kuhofia hatua hiyo na kusisitiza kuwa inajenga ushawishi mkubwa zaidi wa kimkakati kwa manufaa ya China.

Akizungumza katika mkutano wa kilele wa miradi ya miundombinu na ujenzi mjini Beijing, Rais Xi Jinping, alitoa wito kuwa ni wakati mwafaka kwa mataifa zaidi kujiunga na kuyaondolea  wasiwasi baadhi ya watu kwamba mradi huo wa China utazinasa nchi katika madeni makubwa ambayo yatahatarisha uhuru wao.

Xi amesema kwamba mradi huo umelenga kuziendeleza nchi za Afrika na za barani Asia ambazo zimejenga bandari na njia za reli kwa mikopo kutoka China, lakini pia umelenga kutanua wigo kwa mataifa mengine ya Bara la Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini. Katika hotuba yake, Rais Xi aliahidi kuwa nchi yake inadhamiria kuleta faida kwa wote duniani bila kujali nguvu ya mataifa yatakayonufaika.

Mkutano huo wa kilele unaoendelea mjini Beijing unahudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 40, ikiwa pamoja na viongozi kutoka nchi za Afrika.

Duru za kisiasa zimesema kuwa mkutano huo umetafsiriwa kuwa ni vita ya kibiashara kati ya China na Marekani. Vita ya kibiashara baina ya Marekani na China inaathiri pia uchumi wa Ujerumani na Bara la Ulaya kwa jumla. 

Kwa mujibu wa Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Peter Altmaier, amesema kuwa mkutano wa kilele kuhusu mradi wa China wa ujenzi wa miundombinu ya kuyaunganisha mabara, unaofanyika mjini Beijing, Waziri Altmaier amekutana na Makamu wa Waziri Mkuu wa China, Liu He, anayeiwakilisha nchi yake kwenye mazungumzo na Marekani juu ya kuutatua mgogoro huo wa kibiashara.

Aidha, Altmaier amesema kuwa mgogoro huo wa mataifa makubwa kabisa mawili unazuia kasi ya ustawi wa uchumi wa dunia, vilevile mazungumzo mengine baina ya China na Marekani yamepangwa kuendelea wiki ijayo mjini Beijing.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles