24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MIHOGO KUANZA KUZALISHA BIA NCHINI

Na Gabriel Mushi

Kampuni ya Bia nchini (TBL) inatarajia kuanza kutumia zao la mihogo kuzalisha bia ili kuongeza wigo kwa wakulima kupata faida kutokana na kilimo cha zao hilo nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana Agosti 14 na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyaji Tanzania (TDL), Davis Deogratius wakati akiwasilisha taarifa kuhusu utendaji wa kiwanda TBL kwa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iliyotembelea kiwanda hicho.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robert Jarrin, Davis amesema tayari kampuni hiyo imeshaanza kufanya utafiti maalumu kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bia zitokanazo na muhogo.

“Msumbiji tayari wanazalisha bia itokanayo na muhogo, hivyo sisi pia tunaelekea huko katika kupanua soko letu kwa sababu zaidi ya asilimia 76 ya soko la bia na vinywaji vikali bado halijatumika ipasavyo, linatumiwa na hivi vilevi visivyo na ubora kama ‘mataputapu’.

“Lakini serikali iikubali kuandaa mazingira mazuri ya uzalishaji ikiwamo kupunguza kodi na kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyosababisha gharama za uzalishaji kuongezeka hali itaendelea kuwa nzuri kwanisasa tunazalisha bidhaa zetu kwa kutumia, ngano, shayiri, mtama na mahindi,” alisema.

Aidha, kutokana na hali hiyo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwamo Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) alikitaka TBL pia kuanza kufanya utafiti wa uzalishaji wa bidhaa za kampuni hiyo kwa kutumia korosho kwa kuwa mabibo ya korosho hutumika kutengenea gongo.

“Tafadhali pia mzingatie suala la korosho kwa sababu yale mabibo wananchi kule kwangu wanayatumia kutengenezea gongo, sasa ili waondokane na hayo TBL nawalika tuje tushirikiane kwa lolote,” alisema.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mbunge wa Bahi, Omary Badweli (CCM) ambaye aliitaka TBL kuharakisha utafiti huo na kuanza uzalishaji.

“Pia hizi changamoto zilizopo ziondolewe haraka ili muendelee kuzalisha kinywaji cha Value vya kutosha kwa kuwa kinatumia zabibu nyingi kama mlivyosema hakika wakulima wa zao hilo watafaidika.,” alisema

Aidha, Mbunge wa Viti Maalumu Tabora, Munde Tambwe (CCM), ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo alisema tayari TBL inatakiwa kuchangamkia fursa ya mihogo haraka kwa kuwa tayari wachina wameshaagiza zaidi ya tani 100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles